Mhe.Mbunge Viti Maalum (CCM),Hawa Mchafu, Mkoa wa Pwani.
MBUNGE HAWA AHAMASISHA JAMII UNAWAJI MIKONO
NA
VICTOR MASANGU, PWANI
JAMII imetakiwa kuhakikisha kwamba, inajenga tabia ya kunawa
mikono mara kwa mara kwa ajili ya kuepukana na magonjwa mbali mbali ya milipuko
ikiwemo kuumwa na tumbo na badala yake wazingatie maelekezo ambayo yanatolewa
na wataalamu wa afya ili kuupukana na hali hiyo.
Kauli hiyo, imetolewa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,
Hawa Mchafu, wakati alikuwa akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusiana na
masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kujadili, namna ya kuweza kukabiliana
na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yakiwakumba baaadhi ya wananchi.
Mchafu alisema kwamba, kwa sasa nia ya serikali ya awamu ya tano
ni kuboresha huduma ya afya katika maeneo mbali mbali ikiwemo Zahanati, vituo
vya afya, pamoja na hospitali ili kuweza kuwapatia huduma iliyo bora kwa
wananchi sambamba na kuhakikisha kwamba, wanahudumiwa bila ya kupata usumbufu
wowote.
“Kikubwa ninachowaomba wananchi, pamoja na jamii kwa ujumla, ni
lazima tubadilike kwa kuhakikisha kwamba, tunakuwa na utaratibu wa kunawa
mikono yetu katika vipindi tofauti, na tukifanya hivi nina imani kubwa tutaweza
kabisa kuepukana na magonjwa mbalimbali ya milipuko ambayo imekuwa ikijitokeza
katika maeneo ambayo tunaishi, hivyo ni vema tukazingatia mwongozo unaokuwa
ukitolewa na wataalamu wetu wa afya,”alisema Hawa.
Kadhalika, aliongeza kuwa, ni lazima pia wananchi wawe na
utaratibu wa kusafisha maeneo yao mbalimbali ambayo wanaishi pamoja na kufyeka
nyasi na kufikia madimbwi ya maji, ambayo ndio yamekuwa ni chanzo kikubwa na
kusababisha kutokea kwa magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa
kipindupindu.
Aidha, Mbunge huyo, aliahidi kuendelea kushirikiana na wananchi,
pamoja na wataalamu wa afya katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa elimu ya
mara kwa mara, hasa katika maeneo ya vijijini ili kuweza kutoa elimu ambayo itaweza
kuwa ni moja ya msaada na mkombozi mkubwa wa kuwasaidia wananchi kujikinga na
magonjwa ya mlipuko.
Nao, baadhi ya wananchi Wilayani Kibaha, wamempongeza Mbunge
huyo, kwa kuweza kuwatembelea katika maneo yao na kuwapa elimu inayohusiana na
magonjwa ya mlipuko na kwamba maelekezo hayo watayafanyia kazi ili kuweza
kuondokana kabisa na hali hiyo ya kuumwa magonjwa hayo na kwamba
wameiomba serikali ya awamu ya tano, kuwaboreshea huduma zaidi ya matibabu
katika maeneo ya vijijini.

No comments:
Post a Comment