MSAJILI WA BODI YA
NYAMA TANZANIA KUKABILI URASIMU UTOAJI VIBALI
NA
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Uongozi wa
bodi ya nyama Tanzania (TMB) umesema kwamba utahakikisha unaendelea
kushirikiana bega kwa bega na wawekezaji wa viwanda kwa lengo la kuweza
kuwaondolea changamoto zao mbali mbali zinazowakabili ikiwemo suala la
vibali maalum kwa ajili ya kuuza nyama zao katika nchi za njkuingilia kati kwa
kulivalia njuga Sakata la kunyimwa vibali kwa ajili ya kuuza nyama
katika nchi za nje ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Imani
Sichalwe wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Kibaha yenye lengo la
kutembelea baadhi ya maeneo ikiwemo viwanda ili kuweza kujionea shughuli mbali
mbali zinazofanyika pamoja na kubaini changamoto zilizopo ili kuweza kuzichua
na kuzitafutia ufumbuzi.
Pia Kaimu huyo
alibainisha kuwa kwamba kwa sasa wameshaanza mipango ya kuzungumza na
baadhi ya mabalozi wa nchi husika hususan za Uharabuni ili kuona
namna ya kuweza kupata vibali na kuwasaidia wafugaji waweze kupata soka la
uhakik ambalo litawafanya wafugaji pamoja na wawekezaji kuuza nyama yao bila
usumbufu wowote ule.
“Kwa
kweli kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuweka mipango ya kuzungumza
na mabalozi wan chi husika ambao wana mahitaji ya kupata nyama kutoka Tanzania
hususan katika nchi za uarabuni na mchakato huu tayari tumeshaunza na kwamba
mazungumzo pindi yakikamilika yataweza kuwa mkombozi mkubwa kwa viwanda ambavyo
vinachakata nyama kupata soko la uhakika,”alifafannua Msajili huyo.
Katika hatua
nyingine aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuendekea kutoa elimu ya kutosha kwa
wafugaji mbali mbali nchi nzima juu ya umuhimu wa kuzingatia maelekezo mabyo
yanatolewa na wataalamu wa mifugo kwa ajili ya kuweza kuhudumia ipasavyo
ikiwemo kuwapatia chanjo ili kuondokana na changamoto ya mlipuko wa magonjwa.
“Kitu
kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunawaondolea wawekezaji wetu wa
ndani na wale wan je ya nchi changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa
zikiwakabili na kupelekea wakati mwingine kukwamisha malengo
waliyojiwekea katika kukuza uchumi wa nchi na kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuchangia pato la Taifa kupitia sekta ya viwanda,”alifafanua .
Naye Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Vijiji Michael Mwakamo amebainisha kuwa ujenzi wa
kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la kukuza uchumi pamoja
na kuwapatia vijana fursa za ajira na kuondokana na wimbi la umasikini.
Pia Mwakamo
alimpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuhimiza
ujenzi wa viwanda mbali mbali ambavyo vimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
kukuza uchumi wan chi pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ambao
wameweza kunufainika katika suala zima la kujikwamua na wimbi la
umasikini.

No comments:
Post a Comment