Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro(MOROPC ) wamempa dhamana ya kuongoza Klabu hiyo,Bw.Nickson Mkilanya kwa kipindi kingine cha miaka mitano(2020-2025).
hatua hiyo imekuja baada ya wajumbe kufanya uchaguzi wa viongozi wa Klabu hiyo hivi karibuni ambapo Bw.Mkilanya kuomba ridhaa kwa wajumbe ya kuongoza jahazi hilo.
Mnamo Agosti 22,2015,wajumbe wa mkutano mkuu ambao ni wanachama
wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro walifanya uchaguzi wa viongozi
wao waliokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha,viongozi wengine waliochaguliwa kuongoza ni pamoja na
Bw.Ashton Balaigwa,Makamu mwenyekiti,huku nafasi ya katibu mtendaji
imenyakuliwa na Bi.Lilian Lucas ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza kushika
nafasi ya ukatibu toka Klabu hiyo ilipoanzishwa mwaka 1997.
Nafasi ya katibu msaidizi ameipata Bw.Jimmy Mengele ambapo
nafasi ya mwekahazina amechaguliwa BI.Loveness Nyawili ambapo viongozi wengine
waliochaguliwa ni Bi.Hilda Singano,mwekahazina msaidizi huku Bw.Mohamed
Issa,Bw.Severin Blasio na Chistian Kilewa kuwa wajumbe wa kamati tendaji.
katika mkutano huo,mgeni rasmi alikuwa katibu tawala wa mkoa wa
Morogoro,Mhandisi Emanuel Kalobelo ambapo amewapongeza waandishi wa habari mkoa
wa Morogoro kupitia moropc kwamba wametoa mchango mkubwa katika kutangaza fursa
za kiuchumi zilizopo mkoani huko,aliahidi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa
habari wote kwa hali na mali.
No comments:
Post a Comment