WATALII
550 KUTOKA ISRAEL KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA ,TANAPA
Na Lilian Lucas.
WATALII
550
kutoka nchi ya Israel wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa makundi na
nyakati tofauti kuanzia kesho Agosti 2, 2021 kwa ajili ya kutembelea vivutio
vya utalii.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha Agosti 1, 2021, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi
na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA), Pascal Shelutete amesema watalii hao watatembelea Hifadhi za Taifa
zilizopo Kaskazini mwa Tanzania na Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Shelutete amesema kundi la
kwanza lenye idadi ya watalii 150 litawasili nchini kwa kutua katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Shelutete, amesema ujio wa
watalii hao ni matunda ya juhudi kubwa za utangazaji utalii zinazofanywa na
Serikali ya Awamu ya Sita, sambamba na jitihada za makusudi zinazochukuliwa na
serikali hiyo katika kukabiliana na UVIKO-19 (COVID-19) kwa miongozo
inayoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ikiwemo kuhamasisha na
kutoa chanjo ya ugonjwa huo.
Aidha, Kamishina huyo
masaidizi, amesema kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania nchini Israel nako
kumechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la watalii kutoka nchini humo.
Amesema kuwa kuongeza kuwa
mwaka jana Tanzania ilipokea watalii zaidi ya 1,000 kutoka Israel waliokuja
kutembelea vivutio mbalimbali na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka
huu.
Amesema Kesho watalii 150
watashuka, Agost,9 watashuka watalii 200 na Agost16 watalii 200 wengine
watawasili.
Shelutete amesema watalii
hao watatembelea hifadhi za kaskazini na Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment