MASHISHANGA AIPONGEZA SERIKALI, AWAASA WAJUMBE MKUTANO MKUU TFF
Na Thadei Hafigwa
MJUMBE wa.bodi ya Shirikisho.la soka nchini(TFF) ambaye.pia ni mkuu wa mkoa mstaafu Morogoro,stephen.mashishanga ameipongeza serikali kupitia wizara ya habari,sanaa,michezo na utamaduni kuingilia sakata la TFF ulioibuka hivi karibuni ulikuwa na viashiria vya kuzorota kwa programu zake za kiutendaji.
Mashishanga amebainisha hayo mjini hapa wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa uchaguzi wa kugombea nafasi za katika kamati za kiutendaji zilizogawanywa katika kanda 6 ndani ya TFF unaofanyika Agosti 7,mwaka huu jijini Tanga.
Mjumbe huyo wa bodi amesema kuwa hatua ya serikali kutoa msimamo wake wa kuitaka TFF kuendelea na programu zake ni jambo jema na la kupongezwa kwa kuwa.inaendeleza dhamira yake ya kuimarisha na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini
Aidha,amewatakiwa mafakio kwa viongozi watakaochaguliwa kuchapa kazi ili kuendeleza soka hapa nchini,na kuwa wamoja katika kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza katika utendaji kazi wao.
Mashishanga amewaasa pia wajumbe wa mkutano huo kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi kwa kuwapa fursa wagombea wote waliopita kwenye mchujo kujinadi kwa uhuru bila upendeleo.
Alisema mchezo ni furaha,amani na upendo ambapo ni jukwaa la kuwaleta pamoja wadau wa.michezo ili kila mmoja aweze kutoa mchango wake kwa masilahi mapana ya umma.
Hata hivyo,amewataka.wagombea katika nafasi hizo za kiutendaji kuheshimu
na kukubaliana na matokeo yeyote yatakayojitokeza baada ya kupiga kura.
No comments:
Post a Comment