Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia akimpa mkono na
kumkabidhi madawati 60 mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Boko Timiza Fatma Pawa
katika hafla iliyofanyika shuleni hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa
serikali ambayo yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 ambazo
zimetolewa na mfuko wa Jimbo.
VICTOR
MASANGU, KIBAHA
MBUNGE wa jimbo la Kibaha mji
Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika
kuboresha sekta ya elimu ameamua kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwa
kuchangia madawati 220 katika shule tatu za sekondari na moja ya msingi
zilizopo katika halmashauri hiyo ambayo yamegharimu kiasi cha zaidi ya
shillingi milioni 12 ambazo zimetolewa kutoka katika mfuko wa Jimbo.
Koka
alikabidhi madawati hayo kwa wakuu wa shule za sekondaari na msingi ikiwa ni
moja ya utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa kwa wananchi sambamba na
kutekeleza ilani ya chama ambapo amesema kwamba lengo lake kubwa ni
kuweza kuwasaidia walimu na wanafunzi kuondokana na changamoto
walizonazo.
Mbunge huyo
ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya mji Kibaha sambamba
na baadhi ya wajumbe wa mfuko huo wa jimbo alisema kwamba anatambua baadhi ya
wanafunzi katika shule wanakabiliwa na kero kubwa ya kusoma wakiwa katika hali
ya lundikano hiv yo ana imani sapoti hiyo ya madawati itaweza kuleta mabadiliko
chanya kwa wanafunzi kuweza kusomea katika mazingira ambayo ni rafiki.
“Katika
ziara yangu hii lengo langu kubwa ni kutembelea katika baadhi ya shule za
sekondari na msingi ikiwa ni kuunga mkono kwa namna moja ama nyingine sekta ya
elimu na ndio maana kwa kutumia fedha za mfuko wangu wa jimbo nimeweza kutoa
madawati hayo 220 katika shule na hii itaweza kuleta mabadiliko hata kuongeza
kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwani kwa sasa wataweza kusoma katika
mazingira ambayo ni rafiki,”alifafanua Koka.
Katika ziara
hiyo ya siku moja ambayo imefanywa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini
aliweza kutembelea katika maeneo mbali mbali yanayohusiana na sekta ya elimu
ambapo katika shule ya msingi Boko timiza aliweza kukabidhi madawati 60, shule
ya sekondari tumbi viti na meza vipatavyo, 38, shule ya sekondari picha ya
ndege viti na meza 20 ,pamoja na kukabidhi viti na meza 20 katika shule
ya sekondari Kidimu.
Aidha,
Koka alisema moja ya mikakati yake ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na
halmashauri ya mji Kibaha katika kuweka mipango madhubuti ambayo itaweza kuleta
matokeo chanya katika kuboresha zaidi miundombinu ya madarasa, matundu ya vyoo
sambamba na kuwajengea walimu miundombinu bora ya ofisi zao ili kuongeza tija
zaidi katika suala zima ya ufundishaji.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Tumbi Fidelis Haule alimpongeza
Mbunge Koka kwa maamuzi yake ya kutoa sapoti ya madawati katika shule hiyo
kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wanakabiliwa na adha kubwa ya kusoma wakiwa
wamekaa chini hivyo utaweza kuwa ni chachu zaidi ya wanafunzi kufanya vizuri
katika masomo yao.
“Kwa upande
wangu mimi kama mkuu wa Shule hii ya sekondari Tumbi napenda kutoa shukrani
zangu za kipekee kwa Mbunge wetu wa jimbo la kibaha mjini kwa kuweza
kutuona jinsi tulivyokuwa tunauhitaji mkubwa wa viti na mezi lakini kwa
kuwa tumeshapatiwa viti vipatav yo 38 pamoja na meza zake 38 kwetu sisi ni jambo
jema sana katika kuwakomboa wanafunzi kutokukaa chini,”alisema Haule.
Naye
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kihaba, Robert Shilingi alisema kwamba anatambua
mchango mkubwa ambao unafanywa na mbunge koka katika suala zima la kusukuma
gurugumu la maendeleo hususan katika nyaja ya elimu na kuongeza kuwa wataendelea
kushirikiana naye ili kuweza kupiga hatua kwa shule za msingi na sekondari
zilizopo katika halmashauri ya mji Kibaha.
Diwani wa
kata ya Tumbi, Rymond Chokara ambaye shule yake ya Msingi Boko Timiza imeweza
kukabidhiwa jumla ya madawati 60 licha ya kutoa shukrani zake za dhati kwa
Mbunge Koka kwa kuweza kufanikisha ahadi zake kwa vitendo kwa lengo la
kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki na kwamba
amemuomba ombi maalumu katika kata yake waanze mradi wa ujenzi wa shule
ya sekondari ambayo itawaondolea adha wanafunzi ya kutembea umbari mrefu.
Afisa elimu
msingi katika halmashauri ya mji Kibaha Bernardina Kahabuka alisema kwamba
lengo la serikali ni kuendelea kusimamia sera ya elimu bure na kwamba
wataendelea kumpa ushirikiano wa kutosha Mbunge huyo ili kuweza kutimiza
malengo ambayo wamejiwekea na kuwaasa wazazi na walezi kuhakikisha
wanashiriki kikamilifu katika vikao vinavyoitishwa mashuleni lengo ikiwa ni
kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Nao baadhi
ya walimu wa shule ya sekondari Picha ya ndege pamoja na shule ya sekondari
kidimu na wao hawakusita kutoa shukrani zao kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha
mji kwa kuweza kutenga fedha kupitia mfuko wa jimbo lake kwa ajili ya kuboresha
sekta ya elimu na kuwasidia wanafunzi kuondokana na kilio chao cha kusoma
katika hali ya mlundikano.
No comments:
Post a Comment