WANANCHI WA MWANAMBAYA,
MKAMBA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI MKURANGA
VICTOR
MASANGU, MKURANGA
WANANCHI zaidi ya elfu 10 kutoka kata mbili za Mwanambaya na Mkamba zilizopo katika halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya
kutembea umbali mrefu kusaka maji usiku na mchana hatimaye wamepata mkombozi
baada ya kukamilika kwa miradi miwili ya maji safi na salama.
Hayo
yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa maji
Mhandisi MaryPisca Mahundi yenye lengo la kutembelea na kufanya
ukaguzi wa miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika Wilaya ya Mkuranga na
Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) Mkoa wa Pwani.
Katika ziara
yake hiyo, Naibu Waziri amebainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya
awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni
kuhakikisha kwamba inaboresha miundombinu ya upatikanaji wa maji safi na
salama na kuwasadia wananchi wote hasa wakinamama kuwatua ndoo kichwani
pamoja kuondoka na kero ya kutembea umbali mrefu.
“Nipo katika
ziara yangu ya kikazi katika baadhi ya wilaya za Mkoa wa Pwani nimefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga na
kwa kweli nimeweza kujionea miradi miwili mikubwa ya maji ambayo inasimamiwa na
wenzetu wa Ruwasa lakini kitu kikubwa nina imani kwamba wanawake wa maeneo hayo
wataweza kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda
kuchota maji ya kisima,”alisema Naibu Waziri.
Pia, aliwataka
wananchi wote wa Wilaya ya Mkuranga kuunga mkono na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ambao
wanajenga miradi hiyo pamoja na kuhakikisha kwamba wanailinda miundombinu ya
maji isiweze kuharibiwa na wala kuibiwa na badala yake waitunze ili iweze
kudumu kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na mapungufu.
Kadhalika,
aliwapongeza uongozi wa Ruwasa Mkoa wa Pwani na kuwataka waendelee zaidi ya
kufikisha huduma ya maji safi na salama katika maeneo mengine ambayo
yamekuwa na changamoto kubwa ya wananchi kutokupata huduma hiyo na kuongeza
kwamba serikali itaendelea kuweka mipango madhubuti yenye lengo la kutatua kero
za maji kwa wananchi wake.
Katika hatua nyingine aliwataka wakandarasi wote kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kumaliza miradi ambayo wamepangiwa kwa wakati ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kuanza kuitumia miradi hiyo kwa muda ambao umepangwa na kuahidi kuyafuatilia malipo yote ambayo yanadaiwa na baadhi ya wakandarasi.
Naye, Meneja wa Wakala
wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Mkuranga Injinia
Maria Malala amebainisha kwamba kwa sasa kiwango cha upatikanaji wa maji ni
aslimia 76 na kwamba na kwamba wanatarajia kufikisha huduma hiyo kwa
wananchi mbali mbali kutoka kata zipatazo 19 wanazozihudumia.
Kadhalika, alioongeza kuwa katika mwaka wa fedha wa kuanzia 2021
/2022 Ofisi ya Ruwasa Wilaya ya Mkuranga inaendelea na utekelezaji wa miradi
ipatayo sita,ambayo itatumia mfuko wa maji wa (NWF) na kwamba utekelezaji wake
utakusa katika maeneo mbali mbali yakiwemo Mwanambaya,Mkerezange,Msorwa,Mvuleni
Kilimahewa kusini, pamoja na ujenzi wa mradi wa kijiji cha Mdimin ambao
utakamilika octoba 2021.
Nao, baadhi ya wakinamama wanaoishi katika kaya ya Mwanambaya akiwemo pili Rajabu wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na uongozi wa Ruwasa kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa maradi huo ambao kwa upande wao utakuwa ni mkombozi mkubwa sana.
Alifafanua kuwa cha kipindi cha miaka mingi wakinamama hao
walikuwa wanakabili na baadhi yao ndoa za kuvunjika na kuachwa na wanaume zao
kutokana kutumia muda mwingi wakiwa visimani kwa ajili ya kuchota maji
umbari mrefu na kupelekea kuchelewa kurudi majumbani kwao kwa wakati
hivyo wakati mwingine wanajikuta wanapata kipigo.
WAKALA wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa
Pwani kwa sasa inahudumia katika maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo ya Mkuranga
ambapo jumla ya kata 19 na kwamba imefanikiwa kutekeleza mradi mkubwa wa
kusambaza maji safi na salama awamu ya kwanza uliofadhiliwa na Dawasa kwa
Gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 5.5.
No comments:
Post a Comment