Mbunge Koka awafariji Wahanga wa Moto Kibaha
NA VICTOR
MASANGU, KIBAHA
KAYA
zipatazo sita zimenusurika kupoteza maisha yao katika
eneo la mitaa miwili ya Muharakani na Mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani
baada ya nyumba zao walizokuwa wakiishi kupata janga la kuunguliwa
na moto na kusababisha uharibifu mkubwa ambao umepelekea kuteketea kwa
mali zao zote huku wakiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na kukosa makazi
ya kuishi.
Kufuatia
tukio hilo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama
cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ametembelea katika eneo la tukio akiwa
ameambatana na baadhi ya vongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Chama na
kujionea uharibufu ambao umejitokeza ambapo amewafariji wahanga
waliounguliwa na nyumba zao kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1.2
ambazo zitaweza kuwasaidia kujikimu katika kipindi hiki kigumu
walichonacho.
Koka
alibainishwa kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo la moto ambalo limeweza
kuwafanya baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo kuishi
katika mazingira ambayo sio rafiki ndio maana akaamua kuacha mambo mengine kwa
ajili ya kwenda kuwafariji wahanga hao ambao kwa kweli mali zao zote zimetekea
kwa moto na mimi nitaendelea kuwapa sapoti kadiri ya uwezo wangu.
“Mimi kama
Mbunge wenu wa Jimbo la Kibaha mjini tukio hilo la wananchi wangu kupatwa na
janga la moto limenishitua sana na kwamba nilipatiwa taarifa hizi wakati nipo
katika vikao vya Bunge lakini kutokan na hali jinsi ilivyo na wananchi
wamepoteza mali zo na kuunguliwa na vitu mbalimbali imelazimu sasa niache
shughuli zingine ili nije nije kuangalia hali halisi ya tukioa na nimeweza
kuona hivyo nimechangia kiasi cha shilingi milioni 1.2 na huu ni mwanzo tuu,” alisema
Koka.
Aidha,
Mbunge huyo alisema kwamba licha ya kwamba familia hizo zipo katika wakati
mgumu wa kupata janga la kuunguliwa na nyumba zao ataendelea kushirikian nao
bega kwa bega katika kipindi chote cha tatizo hili kwani pamoja na kutoa fedha
hizo lakini bado kuna michango mingine ambayo inahitajika ili wananchi hao
waweze kurejea katika hali yao ya kawaida.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa wa Mtaa wa Muharakani alibainisha kwamba majirani
waliweza kufanya jihihada zote kwa ajili ya kuuzima moto huo ili kuokoa
mali zilizokuwa ndali lakini walishindwa kufanikiwa na kusababisha mali zote
kuteketea na moto huku akibainisha hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha kwani
waliwahi kutoka nje.
“Mheshimiwa
Mbunge kwanza sisi kama wananchi wako tumefarijika sana kwa ujio wako maana kwa
kweli hizi kaya kwa sasa zipo katika mazingira magumu lakini msaada wako huu
utaweza kusaidia kununua mahitaji mbali mbali amabyo ni muhimu maana siku ya
tukio tulijitahidi kupambana kuokoa mali lakini tulishindwa kabisa na gari la
zima moto pindi lilipofika tayari vitu vyote vilikuwa vimeteketea,”alibainisha
Mwenyekiti.
Nao baadhi
ya wahanga wa janga hilo la moto hawakusita kumpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la
Kibaha mjini kwa kuamua kuacha vikao vinavyoendelea Bungeni na kwenda
kuwafariji pamoja na kuwapatia msaada wa fedha ambazo zitaweza kuwasaidia
katika baadhi y mahitaji muhimu na kuiomba serikali na wadau wengine
kuwasaidia msaada wa hali na mali ili waweze kijikimu kimaisha.
“Kwanza
kabisa tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa baba yetu ambaye ni Mbunge
wetu wa Jimbo la Kibaha mjini Koka kwani ni viongozi wachache sana ambao wana
moyo kama wake kwani ameweza kuacha shughuli zake mbali mbali ikiwmeo vikao vya
Bunge ili kuweza kuja kutufariji na kutupa msaada huu hivyo tunamshukuru sana
Mbunge wetu”alisema wahanga hao.
Pia
aliongeza kuwa pamoja na kupatiwa msaada huo lakini kutokana na ukubwa wa tukio
hilo wamesema kwamba bado wahahitaji msaasa wa vitu mbali mbali ikiwemo nguo,
vyakula, pamoja na mahitaji mengine na kuimba serikali kuiliangalia zaidi
jambo hili kwa jicho la tatu kwa lengo la kuwasaidia katika jambo hilo ambalo
limewafanya waweze kurudi nyuma katika kutimiza malengo yao.
Tukio hilo
la janga la moto limetokea hivi karibuni katika mtaa wa Muhazakani pamoja
na mtaa wa mkuza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani na kusababisha nyumba
mbili kuungua na kaya sita kukosa makazi ya kuishi kutokana na mali zote
zilizokuwemo ndani kuteketea kwa moto na kwamba inadaiwa chanzo cha moto
huo ni itirafu ya umeme.
No comments:
Post a Comment