MKOA PWANI WAZIDI KUTOA FURSA KWA WAKEZAJI,WAKUTANA NA WAJUMBE WA CHINA
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo wa kati kati aliyenyoosha mikono akizungumza na baadhi ya wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kupanga mikakati ya ujenzi wa viwanda katika Mkoa huo.
VICTOR MASANGU, PWANI
SERIKALI ya Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo
azma ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuwapa fursa wawekezaji wa
ndani na nje ya nchi imekutana na baadhi Wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba
ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania)
kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi
wa viwanda.
Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
na kuhudhuliwa na baadhi ya viongozi mbali mbali wa Mkoa lengo ikiwa ni kufanya
mazungumzo na wawakilishi hao kwa ambayo yataweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya uwekezaji wa viwanda mbali mbali
ambavyo vikikamilika vitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi katika
kutoa fursa za ajira na kukuza uchumi.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alibainisha
kwamba lengo kubwa la ujio wa wawakilishi hao ni kuweza kutafuta eneo la
ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha
kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo Aprili, 21 mwaka 2021.
“Tumepokea ugeni huu na katika mazungumzo yao ujumbe huo
umekuja kwa lengo kutafuta Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni
kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya
mazungumzo hivi karibuni kwa hiyo sisi kama Mkoa wa Pwani suala hili
tutalifanyia kazi ili kuwapatia ardhi ya kujenga viwanda,”alisema Ndikilo.
Aidha katika
hatua nyingine Ndikilo amewatoa hofu kwa kuwahakikishia wawakilishi
hao wa wafanyabiashara kuwa Mkoa bado una maeneo ambayo tayari
yametengwa maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda hivyo watahakikisha
wanawapa ushirikiano wa kutosha katika kila hatu ili waweze kutimiza malengo
waliyojiwekea,
Pia Ndikilo amependekeza kwa Wawekezaji hao kuwekeza kwenye
eneo la Kwala ambalo Jumla ya Hekta 500 wanazohitaji zitapatikana, na kuwaeleza
kuwa eneo la Kwala linafaa kwa Uwekezaji huo wa ujenzi wa Viwanda
(Industrial Park).
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa katika eneo la Kwala kwa
sasa lina Miundombinu mbinu yote Muhimu ikiwemo, Maji ya uhakika, Barabara,
Umeme wa uhakika ukaribu na Bandari kavu, ukaribu wa Reli ya Mwendokasi, na
ukaribu na Jiji la Dar es salaam.
Wawekezaji
hao wakiongozwa na Bw. Janson Huang wameeleza kuwa wanategemea kujenga na
kuanzisha viwanda zaidi ya 200 vya kuzalisha bidhaa mbali ikiwemo madawa,
Kuunganishia pikiki, Viyoyozi, simu za mikononi hivyo hitaji lao la
kwanza ni Ardhi ila waendelee na michakato mingine ya Uwekezaji
No comments:
Post a Comment