SARAH AWA MISS KITESHE KIBAHA,AHAIDI KUTANGAZA UTALII WA NDANI
Mshindi wa kwanza aliyeibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha wa shindano la kumsaka miss kiteshe 2020 Sarah Zacharia 23 wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tatu bora, kushoto kwake ni mshindi wa nafasi ya pili Zadia Ally huku kulia kwake mshindi wa tatu Zenat Rajab wakiwa pamoja na viongozi walihudhulia katika shindano hilo.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MWANADADA Sarah Zacharia (23) mkazi wa "kwa mathiasi" Wilayani Kibaha
Mkoa wa Pwani ameibuka kidedea baada ya kulitwaa taji la kumsaka miss
Kiteshe 2020 huku nafasi ya mshindi wa pili ikianda kwa Zadia Ally (19) na
nafasi ya mshindi wa tatu ikinyakuliwa na mwanadada Zenat Rajab.
Kutokana na ushindi huo washindi hao watatu wamepata zawadi
mbali mbali kutoka kwa uongozi wa Kiteshe Pub sambamba na kuchaguliwa rasmi
kuwa mabalozi ambao watakuwa na jukumu la kutangaza mbuga ya Nyerere
National park iliyopo Wilayani Rufiji pamoja na vivutio mbali mbali
vinavyopatakana katika eneo hilo.
Mwanadada Sarah Zacharia ambaye ni mshindi wa kwanza katika shindano la miss kiteshe wa kati kati akionyesha ishara ya kumwomba Mungu baada ya kutangwazwa kuibuka kidedea akiwa pamoja na washiriki wengine amabapo kulia kwake ni mshindi wa pili Zenat Rajabu na kushoto kwake ni mshindi wapili Zadia Ally
Katika kinyan’ganyiro cha shindano hilo ambalo lilifanyika
mwishoni mwa wiki liliandaliwa kwa ajili ya dhumuni la kuwasaka walimbwende
watatu ambao watakuwa na jukumu kubwa la kushirikiana na wadau wengine pamoja
na serikali katika kuleta mabadiliko ya kutangaza utalii wa ndani ambao
unapatikana katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani.
Shindaho hilo ambalo liliwashirikisha washiriki wapatao kumi kutoka maeneo mbali mbali lilikuwa na msisimko na ushindano wa aina yake kutokana na warembo wote walikuwa wamejiandaa vilivyo katika staili tofauti na mwonekano mzuri wa mavazi yao ambayo yaliweza kuwavutia mashabiki waliofika katika eneo hilo la Kiteshe kushuhudia mchuano huo ambao umeweza kuacha historia kwa wakazi wa kibaha.
Pia katika shindano hilo warembo hao waliweza kuulizwa
maswali mbali mbali na majaji yanayohusiana na masuala mbali mbali ya utalii
pamoja na mambo mengine ya kijamii ili kuweza kuona upeo wao katika sekta ya
utalii na baadhi yao waliweza kujibu maswali hao kwa umakini hali ambayo
iliwafanya mashabiki waliofika kuweza kupiga mayowe kwa shangwe kulingana na
majibu yaliyokuwa yakijibiwa na walimbwende hao.
Kwa upande wake, Miss Kiteshe Sarah Zacharia ambaye ametwaa
taji hilo alisema kwamba baada ya kuunyakua ushindi huo lengo lake kubwa ni
kuhakikisha anajipanga vilivyo katika kuleta mabadiliko katika kutangaza utalii
wa ndani ikiwemo pamoja na kutoa fursa kwa jamii kuwaelimisha umuhimu wa
kutembelea mbuga mbali mbali za wanyaama ikiwemo ya Nyerere National Park.
“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza
kunifikisha hapa mpaka nimeweza kuchaguliwa kuwa miss kiteshe kwa mwaka huu wa
2020 lakini ndoto yangu kubwa ambayo ninayo ni kuendeleza kufika mbali zaidi
ya hapa katika kutangaza mambo mbali mbali ya utalii wa ndani ukizingatia tuna
mbuga nyingi ikiwemo ile ya Nyerere National Park,”alisema Sarah.
Ni Sarah Zakaria(23) katikakati aliyenasa Miss Kitenge-Kibaha,Pwani
Pia alitoa wito kwa washiriki wenzake ambao hawakuweza kupata
nafasi ya kuibuka kuwa washindi wasikate tamaa na badala yake wahakikishe
wanaendeleza vipaji vyao na fani ya kutangaza utalii wa ndani kupitia fani ya
ulimbwende pamoja na kushirikiana vilivyo na watu wengine ili kutimiza malengo
waliyojiwekea.
No comments:
Post a Comment