Breaking News

Oct 4, 2020

PROFESA KABUDI AWAPA MATUMAINI MAPYA WANANCHI KILOSA

 

Profesa Palamagamba Kabudi Mbunge Mteule,Jimbo la Kilosa,Morogoro
 

Na Mwandishi wetu,Moropc Blog

MBUNGE Mteule kwa tiketi ya CCM,Jimbo la Kilosa,Prof.Palamagamba Kabudi ambaye amepita bila ya kupingwa amewaahidi wananchi wa kilosa, kwamba baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 28,mwaka huu atashughulikia kero 12 zikiwa ni vipaumbele vyake,ikiwemo mafuriko ya mto mkondoa,mgogoro ya ardhi na afya.

Prof.Kabudi amezitaka vipaumbe vyake wakati wa uzinduzi wa hamasa za kampeni cha uchaguzi kwa Wilaya ya Kilosa vilivyofanyika katika viwanja vya Mobonyola-Dumila Oktoba 3 mwaka huu na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa  CCM Mkoa wa Morogoro,Inocent Karogeresi.

Amevitaja vipaumbe hivyo ni changamoto ya ardhi kwa wananchi ambapo atasimamia kwa karibuni  mashamba 49 yalifutiwa umiliki wake na Rais Magufuli ili wananchi waweze kunufaika na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Magufuli katika utatuaji wa kero za wananchi wa Kilosa.

maeneo mengine ni kuhakikisha ya kuwa vijiji 39 vilivyopo Wilaya ya Kilosa,ambavyo havijapatiwa umeme wanaunganishwa umeme,ili kuwarahisishia shughuli zao za uzalishaji kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vitakavyowaongezea vipato vyao katika kukabiliana na umasikini.

Aidha,Profesa Kabudi amegusia suala la ujenzi wa hospitali,vituo vya afya na zahanati kwamba mpaka sasa wananchi wa vijiji 6 Wilayani humo ikiwemo Kijiji cha Kidete hawana zahanati hivyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo huduma ya afya kwa wananchi wa vijiji hivyo wanapatiwa huduma hiyo.

Mbali hayo pia atasimamia ujenzi wa vinara ya simu katika kurahisisha mawasiliano kwa wananchi,ujenzi wa majosho kwa ajili ya mifugo,ili wafugaji waondokane na ufugaji wa kimazoea na badala yake kuwa na mifugo yenye tija na kupanua soko la nyama nje ya nchi hususan nchini Comoro.

Alisema mafanikio hayo yatafikiwa endapo wananchi wakichagua wagombea wa nafasi ya udiwani,ubunge na Urais kupitia chama cha Mapinduzi,kwa kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Dk.John Pombe magufuli katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ilifanya kazi kubwa ya kutukuka katika kuharakisha maendeleo ya wananchi,hivyo Dk.Magufuli ana kila sifa ya kuendelea kuchaguliwa katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Wilaya ya Kilosa ambayo katika Ilani ya chama cha Mapinduzi ni Wilaya ya Kimkakati ina majimbo mawili Kilosa na Mikumi,huku kukiwa na kata 25 kati ya hizo kata 15 wagombea wake wamepita bila ya kupigwa.

Akinadai mgombea wa Kata ya Dumila,Deoglas Mwigumila,Prof.Kabudi amesema mgombea huyo amekuwa shupavu katika ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo hivyo aliwaomba wananchi wa Dumila kumchagua ili awaweze kushurikiana nae katika kutatua changamoto za maji,umeme,afya na elimu.

No comments:

Post a Comment