Paroko wa Parokia ya Tangeni,Padre Emil Kobero akifuatilia kwa karibu wahitimu wa Darasa la Saba (hawapo pichani),Shule ya Msingi Tangeni,iliopo Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro
Na Mwandishi wetu
WAHITIMU wa darasa la saba shule
ya msingi Tangeni,Wilaya ya Mvomero mkoani hapa wametahadharishwa kuwa makini
na maisha ya mtaani baada ya kumaliza elimu ya msingi, kwani kuna uharibifu
mwingi kwa vijana wadogo huku wasichana
wakipata mimba na kutelekezwa.
Wakati wasichana wakipata
mimba wakiwa na umri mdogo kwa upande wa wavulana wakiharibikiwa kwa kujiingiza katika
makundi yasiyofaa hata ya kutumia madawa ya kulevya na bangi.Hivyo,Wazazi nao
wanapaswa kuwaangalia kwa makini watoto wao wakati wakiwa nyumbani baada ya
mitihani yao ya darasa la saba.
Wahitimu wa Elimu ya msingi,Shule ya Msingi Tangeni,Wilaya ya Mvomero,Mkoa wa Morogoro wakionesha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao vya kuhitimu elimu ya msingi kwa mwaka 2020.
Rai hiyo imetolewa na Padre
Emil Deogratias Kobero aliyekuwa Mgeni rasmi katika mahafari ya darasa la saba
wa shuleni ya Msingi Tangeni iliyopo wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro.
Padre Kobero ambaye ni
paroko wa parokia ya Tangeni,mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo Morogoro na
mshauri wa vijana jimbo katoliki Morogoro amesema kuhitimu darasa la saba ni
hatua ya kwenda sekondari hivyo baada ya mitihani yao watoto hao wanapaswa
kupumzika na kujiandaa kwenda sekondari na siyo kujiingiza katika makundi
mabaya au kujihusisha na matendo yasiyofaa au kufanyishwa kazi za kitumwa.
Alisema kuwa, Ushirikiano
wa karibu baina ya wazazi walezi na uongozi wa serikali unahitajika sana katika
kupambana na waharibifu wa watoto, inasikitisha kuona baadhi ya wazazi
wakifumbia macho uovu na ukatili unaotendwa
kwa watoto wao kwasababu ya rushwa wanayopewa na watu wanoharibu watoto hao. Hatua
kali zinapaswa kuchuliwa kwa wazazi wanaoficha uovu huo ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba,Shule ya msingi Tangeni,Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi na walezi wao katika Mahafari ya kuhitimu elimu ya Shule ya Msingi
Akiekieleza zaidi, Padre Kobero
amesema, “tunaishi katika ulimwengu wa utandawazi ulimwengu wa ushindani, elimu
bora ndiyo njia ya kuwajengea vijana uwezo
wa kukabiliana na changamoto za utandawazi hivyo vijana waliohitamu
daarasa la saba wanapaswa kusaidiwa kupata elimu bora ili waweze kufikia ndoto walizo nazo na kuka
biliana na changamoto za utandawazi”.
Naye Mratibu wa Elimu kata
ya Mzumbe akiongea katika mahafari hayo amesikitishwa na ushirikiano mbovu
unaonyeshwa na baadhi ya wazazi linapokuja suala na kuboreha taaluma kwa watoto
wao.
Wazazi walionyesha muamko
kuchangia sherehe ya mahafari lakini siyo kuchangia taaluma. Ila amewahadharisha
wazazi wanaoshirikiana na waharifu wanaowapa mimba watoto wao kwa kumalizana
nao kimya kimya. Hatua kali zitachukuliwa kwa wazi hao.
Akijibu risala ya shule
amabayo ilianisha changamoto za shule zinazoikabili shule hiyo. Paroko huyo
amesema. Ni kweli kuwa shule hiyo ina mapungufu mengi; kwanza madarasa yaliyopo
ni machakavu kwani yalijengwa zaidi ya mika 75 iliyopita pia hayatoshelezi mahitaji.
Hakuna ofisi ya walimu,
kuna upungufu mkubwa wa nyumba za walimu; upungufu wa matundo ya choo, shule haina maktaba wala maabara kwaajili ya
somo la TEHAMA. Hivyo pamoja na hitaji
kubwa la ukarabati wa miundo mbinu iliyopo lazima kufanya jitihada za makusudi
kuweka miundo mbinu mpya.
Katika kukabliana na
changamoto hizo alipendekeza iundwe kamati maalumu ya ukarabati na maboresho ya
shule. Kamati hiyo itakuwa na wajibu wa kuandaa mchanganuo wa mradi mzima wa
ukarabati na ujenzi wa mioundo mbinu
mpya ili kuiweka shule katika hali bora, kuandaa bajeti na kutafuta fedha za
kukamilisha mradi huo.
Kwa mujibiwa risala ya
shule mpaka sasa shule ya msingi Tangeni
ina jumla ya wanafunzi 708, ina jumla ya walimu kumi na moja pamoja na Mwalimu mkuu wa shule na
kati ya walimu hao wa kiume ni wawili (2) na wakike tisa (9). Shule ina vyumba vya madarasa nane
(8) wakati hitaji halisi ni vyuma kumi na sita (16) hivyo kuna upungufu wa
vyumba nane (8) vya madarasa.
Kwa upande wa madawati, shule
inapaswa kuwa na madawi 238 lakini kwa sasa kuna madawai 156 tu hivyo kuna upungufu
wa madawati 82. Kutokana na upungufu mkubwa wa madawati baadhi ya wanafunzi wa darasa la tatu (3),la nne (4) na la tano (5), wanalazimika
kukaa chini hali inayopelekea ugumu katika kujifunza.
Risala imeendelea kunyesha
kuwa shule haina ofisi za walimu na meza za ofisi. Kutokana na ukosefu huo,
walimu wanatumia chumba cha darasa kufanyia shughuli zao.
Wakati huohuo hitaji la nyumba za walimu ni 16, kwa
sasa kuna nyumba mbili tu tena mbovu zinazohitaji ukarabati wa kina.
Akiongea baada ya mahafari
hayo mwenyekiti wa Kamati ya shule ameridhia wazo la mgeni rasmi la kuunda kamati
maalumu kwa ajili ya ukarabati na maboresho ya shule na wajumbe waliopendekezwa
ni pamoja na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi Debora Malyango, Paroko wa Parokia
ya Tangeni Pd.Emil Deogratias Kobero, mwenyekiti wa kamati ya shule, mwenyekiti
wa Kijiji Tangeni, Diwani mteule wa kata ya Mzumbe ,Godfrey Lumongolo na
wajumbe kadhaa wa kamati ya shule.
Pamoja na wajumbe hao kamati
itahusisha watalaamu hasa wa ujenzi na wajumbe wengine watakaoteuliwa na kamati hiyo ya awali.
Shule ya msingi Tangeni
ilianzishwa mwaka 1933 chini ya usimamizi wa Kanisa katoliki parokia ya Mt.
Bernard Tangeni . Mwalimu mkuu wake wa kwanza alikuwa Sista Maria Magdalena (Marehemu).
Baadae shule ilitaifishwa
na serikali lakini bado Kanisa Katoliki parokia ya tangeni linaendelea kuitunza
na kuboresha miundo mbinu ya shule hiyo.
Jumla ya wahitimu 70 waliagwa
katika mahafari yaliyofanyika Oktoba 2,2020.
Hongera sana mwandishi Maalum.Tujumuike kuiboresha shule yetu.
ReplyDelete