“Tumekuwa na mradi
mwingine wa Kijimbo ambapo tumeweza kushirikiana na serikali kwa kujenga jengo
kubwa la kisasa kwa ajili ya kujifungulia wakinamama
ambalo limejengwa pale katika hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi
haya ni moja ya juhudi zangu katika kuboresha afya”Mgombea ubunge Kibaha
mjini(CCM) Sylvestry Koka
Amesema endapo atachaguliwa na wananchi kuwaongoza tena katika kipindi kingine cha miaka mitano atahakikisha analivalia njuga suala la kukabiliana na changamoto inayowakabiliwa wakinamama wajawazito kupoteza maisha wakati wa kujifungua kwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kununua vifaa tiba vya kisasa.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Syvestry Koka wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi kwa ajili ya kuweza kujinadi pamoja na kuomba kura kwa wananchi waweze kuwachaguaSylvestry Koka alimetoa ahadi
wakati wa kampeni ya kuomba kura kwa wananchi wa maeneo ya mbali mbali ya
bundikani katika kata ya Maili moja ambapo amebainisha kwamba nia yake
kubwa ni kuendelea kushirikiana na wananchi na serikali ambayo itaingia
madarakani katika kuweka mazingira rafiki katika utoaji wa huduma ya afya kwa
wananchi husussan wakinamama wajawazito.
Aidha mgombea huyo alibainisha
kwamba kutokana na kuwepo na changamoto ya upatikanaji wa wa utoaji wa huduma
katika baadhi ya maeneo alipambana vilivyo mnamo mwaka 2012 kwa ajili ya kuomba
ujenzi wa mradi wa hospitali mpya ya Wilaya ambapo maombi yake yaliweza kuzaa
matunda kutokana na mradi huo kukamilia.
Mgombe Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka wa kushoto kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) wakiwa sambamba kwenye jukwaa na mgombea udiwani wa Kata ya maili moja Ramadhani Lutambi katika mkutano wa kampeni kwa ajili ya kutoa sera zao kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
“Wakati nipo katika nafasi
yangu ya Ubunge mnamo mwaka 2012 niliomba ujenzi wa hospitali ya Wilaya lakini
alivyoingia katika kipindi kingine aliweza kupambana kutokana na kuona kuna
umuhimu mkubwa wa hospitali hiyo ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa
wananchi kupatiwa matibabu yao kwa urahisi na kwamba kwa sasa hospitali
hiyo imekamilika na tayari imeshaanza kutoa huduma,”alisema Mgombea huyo.
Kadhalika Koka amesema kuwa katika kuboresha sekta ya afya wakati akiwa Mbunge alishatoa msaada wa vifaa tiba mbali mbali katika kituo cha afya cha Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi katika suala zima la upatikanaji wa dawa ili wananchi waweze kupata matibabu bila usumbufu wowote.
Mmoja kati ya makada wa chama cha mapinduzi Mjema wa kushoto akiwa amesimama jukwaani huku amemshika mkono kwa ajili ya kumanadi mgombea udiwani wa Kata ya Maili moja, Ramadhani Lutambi wa kulia katika mkutano wa kampeni amabo ulifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Bundikani.Akizungumzia kuhusiana na suala
la mipango yake katika kuboresha sekta ya afya aliongeza kuwa anatambua
bado kuna baadhi ya maeneo mengine kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma ya
aafya hivyo amewaomba wananachi waweze kumpatia ridhaa ya kuongoza katika
kipindi kingine ili aweze kumalizia utekelezaji wa ilani ya chama katika kuwahudumia
wananchi wote bila ya ubaguzi.
Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya Maili moja
kupitia tiketi ya ( CCM) Ramadhani Lutambi amewaahidi wananchi wa Maili moja kwamba
lengo lake kubwa ni kuhakikisha anasimama kidete katika kusimamia
miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya barabara
pamoja na kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga na kukarabati madarasa
katika shule za msingi na sekondari.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha
mapinduzi katika Halmashauri ya mji Kibaha Maulid Bundala ametoa angalizo kwa wananchi
kuhakikisha wanafanya maamuzi yaliyo sahihi kwa kuwachagua viongozi
wanaotokana na CCM wenye uwezo wa kusikiliza kero za wananchi na
kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment