VICTOR MASANGU,KIBAHA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la
Kibaha Mji kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Slvestry Koka ameahidi
kuwaondolea changamoto wafanya biashara kwa kuhakikisha wanapata maeneo maalumu
kwa ajili ya kufanyia shughuli zao mbalimbali za kibiashara ili waweze
kujikwamua na wimbi la umasikini.
Mgombea huyo Ametoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni
uliofanyika katika viwanja vya maili moja vilivyopo Kibaha mji ambao ulihudhuriwa
na viongozi mbalmbalii wa chama cha CCM pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
Koka aliongeza kuwa katika kipindi kilichopita aliweza
kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kufanikisha miradi mbalimbali
ya maendeleo na kwamba aliweza kufanikiwa kupata mradi mkubwa wa ujenzi wa soko
la kisasa ambalo limeshaanza kujengwa.
“Kikubwa ambacho ninawaomba wananchi wenzangu wa jimbo la Kibaha
mji naombeni kwa moyo mkuchufu kuweza kuniamini tena katika kipindi kingine niwe
mwakilishi wenu katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niweze
kuzitafutia ufumbuzi changamoto zetu kwa kushirikiana na serikali,”aliahidi
Mgombea huyo.
Aidha, alisema kwamba anatambua kuna baadhi ya wafanyabishara
wanafanya shughuli zao katika mazingira magumu na wengine hawana eneo maalumu
kwa ajili ya kufanyia shughuli zao za biashara.
Hivyo
lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaweka
mipango madhubuti ambayo itasaidia kuendesha biashara bila ya kuwepo kwa usmbufu
wowote.
Mwonekano wa baadhi ya
wanachama na wakeleketwa wa Chama cha mapinduzi (CCM) wakiwa wamebeba mabonga
ya picha mbali mbali ikiwemo za Mgombea Urais Dk. Jihn Pombe Magufuli na
nyingine zikiwa za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Slvestry Koka wakati
wa mkutano wa kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi.
“Mimi kwa kweli nina imani kuna mambo mengi ambayo nimeweza
kuyatekeleza wakati wa kipindi changu cha Ubunge kwa hiyo ninaomba wananchi wa
Jimbo la Kibaha mjini tuendelee kushirikiana bega kwa bega ili miradi mingine
ambayo bado haijakamilika iweze kukamilika na nina imani kubwa soko ili kubwa
la kisasa pindi likikamilika litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa
wafanyabiashara,”aliongeza Koka.
Katika hatua nyingine mgombea huyo alisema kwamba serikali ya
awamu ya tano ambayo inaongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imeweza kufanya
mambo makubwa kutokana na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itaweza
kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto
mbali mbali.
Kwa upande wake Mke wa Mgombea huyo Mama Selina Koka hakusita kuwaomba wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini kuweza kumpata nafasi nyingine mume wake ili aweze kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo lengo ikiwa kupiga hatua zaidi katika sekta mbali mbali.
“ Kwa heshima kubwa kwa kweli naweza nikasema serikali ya awamu
ya tano imeweza kufanya mambo mengi sana lakini kitu kikubwa naomba muendelee
kumuamini mume wangu aweze kupata kura nyingine katika uchaguzi mkuuu ambao
unatarajiwa kufanyika Octona 28 mwaka huu hivyo imani yangu mtaweza kumpatia
kura nyingine za ndio,”alisema Mama Selina Koka.
No comments:
Post a Comment