NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi amewahidi
wananchi kuwaletea maendeleo kwa kasi ikiwa ni moja ya mkakati wa utekelezaji
wa Ilani ya chama chake katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Wakati
mgombea huyo wa ubunge akitoa ahadi hiyo,Nae mgombea Udiwani kata ya Mkuza kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Fokasi Bundala amewaomba wananchi
kumuamini na kumchagua kuongoza kata hiyo ili akamilishe miradi aliyokuwa akiisimamia
katika awamu iliyopita.
Wakiwa katika majukwaa wagombea hao wamewahakikishia wananchi mjini Kibaha katika siku ya uzinduzi wa kampeni zao, kwamba, wapo tayari kuwatumikia
wananchi usiku na mchana bila ya ubaguzi wa aina yoyote
Wamejinadi, kwamba kupitia chama cha mapinduzi wananchi wanapaswa kuamini
maendeleo hupatikani kwa ushirikiano hivyo kwakua awamu iliyopita kuna miradi
iliyoibuliwa na bado haijakamilika utekelezaji wake wanaomba tena kupewa nafasi
ili wakasimamie fedha kutoka Halmashauri za kukamilisha miradi hiyo.
Kwa
mujibu wa Ilani ya CCM Katika awamu iliyopita Shilingi billion 5.2
zilitumika katika kata ya Mkuza kutekeleza
miradi ya maji, Elimu, barabara na ujenzi wa Zahanati.
No comments:
Post a Comment