Breaking News

Dec 22, 2024

'MSOUTH 'Atoa Zawadi ya Mavazi kwa Wazee 110 Kingolwira


Valentino Nyefwe (msouth)kushoto akimkabidhi  Diwani wa Kata ya Kingolwira Madaraka Bidyanguze mfuko uliohifadhia msaada wa nguo kwa ajili ya wazee wa Kata hiyo. 

Na Thadei Hafigwa

WAZEE wa Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro wamejikuta wakibugujikwa na machozi ya furaha baada ya kupokea msaada wa mavazi ya aina mbalimbali kutoka familia ya Valentino Khan Nyefwe (msouth).

Katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa nguo ulitolewa na familia ya msouth

Diwani wa Kata ya Kingolwira,Madaraka Bidyanguze  amesema kuwa wazee wa Kata yake ni watu wenye tabia njema,wenye busara na wenye moyo wa shukran  pia ni wacha mungu.

Katibu wa Baraza la wazee Kata ya Kingolwira, Scolastica Mluge (kulia) aliyevaa vazi la rangi ya bluu akiendesha zoezi la kugawa nguo kwa wazee.Katikati ni mdau wa maendeleo Valentino Nyefwe akishuhudia zoezi hilo.

Bidyanguze akitoa shukran kwa niaba ya wazee wa Kingolwira amesema ofisi ya Kata inatambua mchango wa hali na mali inayotolewa na msouth kama mdau wa maendeleo katika kusukuma maendeleo mbalimbali ya wananchi.

Alisema kuwa msouth wakati mwingi amekuwa na moyo wa aina yake kwa kuonesha utayari nyakati zote bila ya kuchoka.

Baadhi ya wazee walioshiriki katika hafla ya utoaji wa Zawadi ya Mavazi kwao iloyotolewa na mdau wa maendeleo,Msouth(Valentino Nyefwe)

Valentino Nyefwe alikingozana na familia yake walitoa msaada wa nguo kwa wazee wa Kata ya Kingolwira 110,ambapo Uongozi wa Baraza la Kata ya Kingolwira,Scolastica Mluge na msaidizi wake Iddi kamandwa uliratibu wa kuhakiki wazee kwa kuwashirikisha viongozi  wa serikali za mitaa 8 iliopo kwenye Kata hiyo.

Sehemu ya familia ya mdau wa maendeleo,msouth(Valentino Nyefwe) walusaidia zoezi la Ugawaji wa Zawadi ya nguo kwa wazee wa Kingolwira)

Katibu wa wazee Scolastica Mluge alitaja mitaa hiyo ni Shule,zahanati, tambukareli,seminari,tenki la maji na mtaa wa mahakamani.

Kwa upande wake msouth alisema yeye na familia yake wamewiwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Kingolwira kupitia ofisi ya diwani.

Diwani wa Kata ya Kingolwira, Madaraka Bidyanguze akizungumza kwenye hafla ya Ugawaji wa Zawadi ya nguo kwa wazee wa Kingolwira 

Alisema kuwa,mara kwa mara amekuwa akiguswa na kuwapwnda wazee kwa kuwa wakati wakiwa na nguvu walimwaga jasho lako katika ujenzi wa Taifa hivyo kwa kuwa wameishiwa nguvu wanapaswa kusaidiwa kwa hali zote ikiwemo mavazi,makazi,chakula na matibabu.

Wazee wa Kingolwira walioshiriki kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi ya nguo

"baadhi yenu tumewasaidia katika kupata bima ya afya pamoja na makazi,kwa mtazamo wangu nimeona ni jambo jema nilipochukua uamuzi wa kumjengea nyumba Mzee mmoja ili aweze kupata mahali pa kuishi badala ya kumpa fedha."alisema.

Alisema kuwa ataendelea kuwasaidia kwa kadri mungu atakavyomjalia,huku akionesha utayari wake wa kukubali kuwa mlezi wa wazee baada ya kuombwa na Uongozi wa Baraza hilo la wazee Kata Kingolwira.

Dec 14, 2024

PSSSF yawajengea uwezo Waandishi wa Habari Morogoro

 


Na Thadei Hafigwa,Morogoro

Uongozi wa chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (MoroPC) umetoa pongezi kwa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi na watumishi wa umma(PSSSF) kwa kuandaa Fursa ya mafunzo kwa Waandishi wa Habari mjini hapa.

Mwenyekiti wa MoroPC,Nickson Mkilanya alibainisha hayo Desemba 14,2024 katika mafunzo kwa Waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro.

Nickson Mkilanya, mwenyekiti MoroPC akieleza umuhimu wa mafunzo hayo.

Mkilanya alisema kuwa Waandishi wa Habari wa Morogoro wapo tayari kushiriana na PSSSF katika kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari juu ya huduma zinazopatikana na kutolewa na mfuko huo nchini.

Alisema kuwa PSSSF isihofu kufanyakazi na mwandishi wa Habari yeyote aliopo mkoani Morogoro Lakini itakuwa vizuri shughuli hizo zikapitia kwenye Klabu ya Waandishi wa Habari ili kuleta tija na ufanisi.

Waandishi wa Habari mjini Morogoro Wakishiriki katika mafunzo.

mmoja wa Waandishi wa Habari wakongwe,ambaye pia ni mnufaika na mfuko huo, Bujaga Izengo Kadago alitoa ushuhuda juu ya huduma bora ya utoaji wa mafao ya kuustaafu inayotolewa na mfuko huo.

Bujaga amesema kuwa baada ya kuustaafu kwake katika utumishi wa umma alifuatilia mafao yake, kwa mterezo bila ya kuwepo na vikwazo ambapo mafao yanatolewa kwa wakati.

Kwa upande wake,Meneja wa mawasiliano na utoaji elimu kwa umma PSSSF,Yesaya mwakifulefule alisema kwa sasa Wana mkakati wa kuelimisha umma kwa kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari Nchini kupitia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani ili kupanua Wigo wa uwelewa kwa jamii na umma.

Meneja wa mawasiliano na utoaji Elimu kwa umma,Yesaya mwakifulefule alisisitiza jambo katika mafunzo kwa Waandishi wa Habari,mjini Morogoro.

Pia,Waandishi wa Habari katika mafunzo hayo walipata fursa ya kukuuliza maswali jinsi ya mfuko huo ulivyojipanga katika mfumo wa kidigiti kwa wanachama wake waliopo vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya tehama 

Mwakifulefule  alisema mfumo huo umejipanga vizuri na changamoto ya tehama ambayo hapo awali ilikuwa ikiwasimu wanachama wa mfuko huo,lakini kwa sasa kero hiyo imekupungua na wanachama wanaridhishwa na huduma.

Picha ya pamoja iliyowashirikisha Waandishi wa Habari na maafisa wa PSSSF mara baada ya. Mafunzo.

Alisema kuwa mafunzo hayo ni endelevu yanaendelea kutolewa ili kuyafikia makundi yote bila ya kumwacha mtu yeyote nyuma katika falsafa ya PSSSF kiganjani ia  yatatolewa kwa awamu kwa kadri ya mahitaji na utekelezaji wa mpango mkakati wa utoaji elimu kwa umma juu ya mfuko huo.

Dec 10, 2024

SERIKALI KUENDELEA KUFUNDISHA WANAFUNZI VYUO VIKUU MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

 


Na Thadei Hafigwa Morogoro
SERIKALI imesema kuwa kupitia wizara ya elimu sayansi na teknolojia inajitahidi kuhakikisha inatoa elimu inayotolewa sasa inaendena na mabadiliko ya teknolojia duniani ili kurahisisha maendeleo nchini bila ya kuachwa nyuma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Daniel Mushi alisema hayo wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la Taaluma ya Maendeleo linalohusisha Vyuo Vikuu vya ndani na Nje ya Nchi linalofanyika mjini Morogoro.
Profesa Mushi alisema kuwa iwapo teknolojia ikitumika vibaya inaweza kuiharibu jamii,pia ikitumika vizuri inaweza kuinufaisha jamii,kwamba njia sahihi ni wananchi kuelimishwa na kushirikishwa dhana sahihi ya maendeleo kupitia wataalam.
“Maendeleo ya nchi hayapatikani bila kuwepo na ushirikishwaji,serikali ina kushirikiana na sekta binafsi,wadau wa maendeleo kwa kuunda utatu wa maendeleo” alisema.
Alisema kuwa katika ushirikiano huo kila upande unapaswa kuwa na dhana sahihi ya maendeleo ambapo kongamano la Morogoro ni kujengeana uelewa sahihi wa kuweza kushirikishana katika utatu wa kuleta maendeleo.

Washiriki wa Kongamano la kimataifa wakifuatilia hoja kutoka kwa watoa mada mbalimbali

Alisema kuwa katika kongamano hilo litakuwa na majawabu ya namna bora ya kuweza kuwafundisha wanafunzi vyuoni ili aweze kuwa na mtazamo sahihi wa dhana maendeleo.
Alisema kuwa dhana ya maendeleo inabadilika kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia,ikiwemo akiliumba(mnemba) katika kujifunza namna ya kutofautisha kazi iliyoandikwa na mwanafunzi kwa kutumia uwelewa wake na utashi wake na ailiyopita kupitia akiliumba.
Kwa upande wake,Profesa William Mwegoha, Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe(MU)  alisema Kongamano hilo linaangalia mfumo na muktadha wa taaluma za maendeleo katika ulimwengu unaoendelea kubadilika katika kiazazi cha sasa na kijacho ili kuleta matokeo chanya.
Profesa Mwegoha alisema kuwa mkutano huo umebeba lengo la kuangalia taaluma za kimaendeleo katika ulimwengu wa mabadiliko ,ikiwemo teknolojia,uchumi na changamoto mbalimbali ,mabadiliko ya tabianchi sanjali na kufanya mapitio katika taaluma za maendeleo zipitiwe ili ziendelee kuwa na thamanika.
Profesa Elizabeth Lulu Genda ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo chuo kikuu Mzumbe, ,alibainisha kwamba ni kongamano hilo ni la tatu la kimataifa limekuwa na mijadala ya kujadili maendeleo kwa kadri ya nyakati na mwaka husika.
Kongamano hilo la Kimataifa  limeandaliwa kwa  ushirikiano wa Vyuo Vikuu vitano,ikiwemo Chuo kIkuu Mzumbe,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,(UDSM),Chuo kikuu Dodoma,Chuo Kikuu cha Afya(MUHAS) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) ikiwa na mada 70 zinazotolewa na wataalamu mbalimbali ndani na nje ya nchi likiwa na kauli mbinu isemayo,mtazamo wa kitafiti wa  Maendeleo kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Nov 23, 2024

Siku 16 za Kupinga ukatiki wa Kijinsia

https://drive.google.com/file/d/1NX_DwFk0lD1rKukmBpV_2VLgNPYoXQp_/view?usp=drive_link

Nov 15, 2024

MADEREVA WATAKA MIKATABA YA AJIRA KUPITIA MDAG

 MADEREVA WATAKA MIKATABA YA AJIRA  KUPITIA  CHAMA CHA MADEREVA MDAG

Na Mwandishi wetu

ILI kukabiliana na matukio ya vitendo vya uharifu,wizi chama cha madereva wametaka wamiliki wa vyombo vya usafiri kushirikiana na chama cha madereva nchini katika uandaaji wa mikataba ya madereva ili kuepuka usumbufu wanaopata wamiliki kwa matukio ya wizi.

Wito huo umetolewa na rais wa Chama cha madereva cha Mkombozi,Seleman Idd (MDAG) katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa matukio ya madereva kuwekwa mahabusu kwa madai ya wizi wa mafuta na mizigo yanasababishwa na uwepo wa mazingira yasiyo rafiki yaliopo mikataba ya ajira zao.

Idd alisema kuwa muarobaini wa matukio ya wizi ni chama chake cha MDAG kukaa meza moja na umoja wa wamiliki wa magari (TATOA) ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo kabla ya dereva hajaanza kazi inapaswa mikataba hiyo ikipitie kwa chama cha madereva ili kulinda masilahi ya pande zote mbili.

alisema kuwa  wamiliki wa magari wanapotaka madereva walipitie kwenye chama,hali hiyo itasaidia kupunguza malalamiko yaliopo kutoka kwa wamiliki wa magari kuibiwa mafuta na mizigo inayosafirishwa.

Hata hivyo alisema mbali ya kuwepo chama cha madereva lakini Chama cha TATOA ambacho nikihusisha wamiliki wa magari ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. “madereva wengi wanatambua kwa nini matukio ya wizi yanatokea,ni wapi wanapotokea wizi.chanzo kikuu ni madereva kukosa stahiki zao kwa wakati.”alisema

Alisema kuwa madereva wanafanyakazi katika mazingira magumu,kwamba malipo wanayopata yamegumikwa na utata kwa kuwa wanasafiri bila kupewa staiki zao kwa wakati,wanatoka Dar es Salaam bila ya kuwa na malipo wanalazimika kuegesha gari wakiwa njia,Morogoro,Dumila wakisubiri kuingiziwa fedha za safari  kwenye simu  hali hiyo imekuwa ni kero kubwa.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili madereva ni pamoja na  kuwekwa mahabusu ndani na nje ya nchi kwa makosa mbalimbali, kutokuwa na bima ya afya,mfuko wa jamii,bima ya kifo na bima ya ajali. kwamba iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa madereva wataendelea kuteseka pamoja na familia zao.

“Madereva wengi wapo mitaani wamevunjika miguu,wengine wamepoteza maisha kutokana na kukosa bima ya ajali,kifo kwamba wanateseka sana wamekuwa omba omba.”alisema. 

Alisema kuwa wadereva wanategemea malipo yao ili kuwahudumia watoto wao,kwa kuwalipia ada,matibabu pamoja na mahitaji mengine ya msingi lakini kwa sababu ya hali ilivyo sasa kuna haja ya vyama viwili kukaa meza moja TATOA na MDAG ili kuboresha masilahi ya madereva ambao kazi yao ni ya hatari.

Nov 5, 2024

Chama Cha MDAG Wapongeza Jeshi la Polisi


Seleman Idd,Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Madereva(MDAG)

Na Mwandishi wetu

Chama Cha Madereva Cha Mkombozi Driving African Group (MDAG) wamelipongeza Jeshi la Polisi Chini kwa kazi nzuri ya usimamizi wa Sheria ya usalama barabarani ambapo imesaidia kupunguza ajali barabarani,hapa nchini.

seleman Iddi ni rais wa umoja wa madereva hao(MDAG) ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambapo blog hii ni miongoni mwa waliofanikiwa kupata taarifa hii, kwamba madereva licha ya kukabiliwa na  changamoto nyingi katika utendaji wao wa kazi kutokana na kufanyakazi zinazohatarisha maisha yao lakini wana Imani kubwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika kuweka mazingira rafiki katika uendeshaji wa Nchini kutokana na falsafa yake ya 4R.

Idd amesema kuwa madereva wengi wa malori hawana mikataba ya kazi,bima kwamba hata malipo wanayopewa ni madogo hayakidhi mahitaji ya kuwasaidia wao na familia zao.

"Sisi tunalipwa mishahara na waajiri wetu kati ya 300,000 hadi 500,000 ,posho ya safari ni kati 700,000 Hadi 800,000 hii haitoshi ukiringanisha na kazi tunazifanya,tunasafiri nje ya nchi,congo na nchi nyingine huko wanatumia Dola,sisi mabosi wetu wanatupa fedha za hapa nyumbani,hii ni changamoto kubwa kwetu" alisema

Alisema kuwa kupitia chama chao wanapendekeza kuwa malipo kwa madereva wa maroli wanaosafiri nje ya nchi walipwe mshahara wa Dola 500 sawa na shilingi mil 1.3 kwa fedha za kitanzania,sanjali na kupatiwa posho katika mfumo wa malipo kwa dola 200 Hadi Dola 300 ya safari ili kuwarahisishia gharama za maisha wanapokuwa nje ya nchi 

Aidha,alisema kuwa chama chao Cha  MDAG nimependekeza mshahara na posho zao zilipwe na waajiri wao(mabosi),kwamba Wana Imani kubwa na serikali kwamba changamoto wanazopata  zinapatiwa ufumbuzi.

Alisema kuwa serikali ikifuatilia na kusimamia mifumo hii ya mikataba kwa madereva wa maroli itakuwa imemaliza tatizo hilo la ambalo amedai ni la muda mrefu.

Sambamba na hayo,alisema kuwa jamii inapaswa kuuelewa na kutambua mchango wa madereva katika sekta ya usafirishaji katika ulinzi na usalama kwenye sekta ya miundombinu,kwamba wapo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na mamlaka zake zote.

Oct 26, 2024

KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA YAWASOGEZEA HUDUMA WATEJEA SGR MOROGORO

Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba(katikati) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Paschal Kihanga aliyevaa shuti kushoto,mara baada ya uzinduzi wa Duka la Airtel lililozinduliwa ofisi ya SGR kituo cha Morogoro(Picha na Thadei Hafigwa)

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

IMEELEZWA kuwa uwepo wa treni ya kisiasa ya SGR imeongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya mawasiliano baada ya kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kujitokeza kuunga mkono serikali kwa kuweka huduma zao kwenye zao kwenye kituo cha Morogoro.

 Sambamba na hiyo, halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inakusudia kuanza ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa ili kuwapunguzia mzigo wa gharama wasafiri wanatumia usafiri wa Treni ya Mwendokasi (SGR) takribani kasi yake kuongeka.

Meya wa Manispaa wa Morogoro,Pascal Kianga alisema ujenzi wake utaanza wakati wote kuanzia sasa baada kupatikana kwa Mkandalasi na kwamba ametaka wakazi wa Manispaa hiyo kutumia fursa ya kuwepo  kwa Treni ya SGR kwa kubuni biashara mbalimbali zitakazo waingizia kipato.

Meya Kianga alisema hayo wakati akizindua Duka la Kisasa la Kampuni ya mawasiliano ya Simu ya Airtel Tanzania  lilojengwa kwenye stendi hiyo ya SGR kwa ajili ya kurahisha wasafiri wanaingia na kutoka nje ya mkoa wa Morogoro.

Mwigizaji wa filamu na michezo ya runinga kutoka nchini Tanzania,(Joti) watatu kutoka kushoto ambaye pia ni balozi wa artel Tanzania,akishuhudia zawadi iliyotolewa na kampuni hiyo kwa Diwani wa Kata ya Kimamba 'B',Willie Mathew wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel katika kituo cha Treni ya Kisasa SGR kituo cha Morogoro,wengine walishuhudia zoezi hilo ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Pascha Kianga,na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Tanzania,Adriana Lyamba.(Picha na Thadei Hafigwa)

Inakadiriwa kuwa wasafiri zaidi ya 1000 wanatumia treni hiyo ya kisasa kwa siku huku wakiwa na mahitaji mbalimbali ya huduma ya mawasiliano.

Alisema fursa nyingine ni pamoja na Manispaa hiyo kuanza kujipanga kuwa Jiji tarajiwa kwakuanza kuboresha miundo mbinu ya mawasilino yatakayorahisha wananchi kupata huduma za kijamiii.

“Niwaombe  wananchi kuchangamkia fursa iliyopo ya SGR inayofanya safari zake Morgoro Dar es Salaam na Dodoma kwa siku kuna abiria zaidi ya 10000 wanaingia na kutoka wanakuja kuanzia safari hao kwenda mikoa mbalimbali watumiea nafasi hiyo kujipanga kufanya shughuli za ujasilimali wasisubiri waje kutoka nje ya mkoa wakati wao wapo hapahapa” alisema Meya Kianga

Alisema Manispaa imeboresha miundombinu ya mawasiliano ambayo kati ya Kata 29 mpaka sasa ni kata moja tu yenye changamoto hiyo ambayo siku chache zijazo tatizo hilo litamalizika.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania,Adriana Lyamba,alisema wameamua kuwasogezea huduma wasafiri wanaotumia Treni hiyo ya Mwendokasi kwenye stendi hiyo ili kupata huduma zote wakiwa kwenye maeneo bila kwenda mjini.

Alisema Airtel imekuwa ikiunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali ikiwemo kusogeza huduma kwa wananchi ili kuwapunguzia adha ya kutumia umbali mrefu kuzifuata huduma hizo.

Katika hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Lucas Lazaro Mhuvile (Joti),mwigizaji wa filamu na michezo ya runinga kutoka nchini Tanzania ambaye ni Balozi wa kampuni ya Airtel Tanzania.

Joti ambaye akiwa balozi wa kampuni ya Airtel Tanzania,amewahimiza watanzania kuhakikisha wanatumia huduma kedekede zinazotolewa na Kampuni hiyo kutokana na jinsi inavyojipambanua katika utoaji wa huduma kwa kuwa karibu na wateja

Oct 18, 2024

KAMPENI BONGE LA MPANGO BENKI NMB YAJA NA ZAWADI NONO


Na Thadei Hafigwa,Morogoro

KATIKA kukabiliana na changamoto za matukio utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wasio na uadilifu jamii imeaswa kuhifadhi fedha katika taasisi za fedha.

Meneja wa benki ya NMB, tawi la Wami, Victor Mboya ,amebainisha hayo katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa baadhi ya wateja wao wanaotumia taasisi hiyo katika uhifadhi wa fedha.

Mboya amesema taasisi hiyo ina wajibu wa kutoa elimu ya kutunza fedha kwa wasio wateja wao.Kwamba watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea kidogo kidogo kwa matumizi ya baadae.

Meneja wa huduma kwa wateja Benki ya NMB tawi Wami,Victor Mboya akimkabidhi Amosi Mayila (aliyevaa t shirt ya rangi ya machungwa)zawadi ya TV inchi 75 baada ya kuibuka mshindi katika droo ya 4.

Amesema kuwa benki ya NMB baada ya kuona umuhimu wa kuweka akiba katika taasisi yao,wameamua kuweka zawadi ili kuhamasisha wateja kuendelea kuweka akiba kupitia kampeni ya bonge la mpango mchongo ndio huu.

Amosi Mayila (22) mkazi wa Ruaha Mkoani Morogoro pamoja na George Ambukege (32) ni  baadhi ya wateja waliokabidhiwa Tv inchi 75 friji kutoka benki ya NMB baada kuibuka mshindi katika droo ya nne.

Aidha,kwa upande wake Amos Mayila ambaye alipokea zawadi ya TV inchi 75 amesema ataitumia zawadi hiyo kama moja ya chanzo cha kujiongezea kipato katika familia yake.

Washindi wengine Shila Gabriel(Manyoni),Joseph Mollel(Singida) na Regins chiwa ambalo kila mmoja katika droo hiyo walijipatia kitita cha shilingi laki moja.

Katika kampeni hiyo mshindi wa jumla atajishindia kitita cha shilingi milioni mia moja na zawadi nyingine mbalimbali ikiwemo friji,mashine ya kufulia na jiko la gesi.

Kampeni hiyo imeanza septemba 25 ambayo itakuwa ni kipindi cha miezi mitatu na inatarajia kuhitimika Desemba 19 mwaka huu.

Oct 16, 2024

Kumbukumbu za kitaifa

 Picha kwa mujibu wa Mkurugenzi ya mawasiliano ikulu






Rais Mwinyi Atoa pole kwa msiba

 


Na Mwandishi Maalum

RAIS MWINYI ATOA POLE KWA MSIBA WA THEREZA OLBAN NYUMBANI KWAKE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amehudhuria msiba wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Marehemu Bi. Thereza Olban Ali, nyumbani kwake Miembeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.



Rais Dk. Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki.

Marehemu Bi. Thereza, wakati wa uhai wake, alikuwa mwalimu na baadaye alijiunga na Chama cha Afro Shirazi (ASP) na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Halikadhalika, aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba mwaka 1983 na alihudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM na Jumuiya zake.

Wananchi wahamasika kujiandikisha daftari ya kumpigia kura

 Uandikishaji wa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani Kilosa ukiendelea. Zoezi hili limeanza Oktoba 11 hadi 20, 2024 ikiwa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024


Oct 14, 2024

Rais wa UTPC ajisajili daftari la wapiga kura

 


Habari kwa hisan ya Sekretaeti ya UTPC

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Bw. Deogratius Nsokolo, amejiandikisha katika daftari la wakazi katika kitongoji cha Kabatini kijiji cha Isinde katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoani katavi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu. 

Baada ya zoezi hilo, Bw Nsokolo ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka watakaosaidia kuleta maendeleo katika maeneo yao.