WIZARA YA ELiMU YATENGA MIL.50 KUCHAGIZA 'MASOMO YA SAYANSI'
Na Thadei Hafigwa
KATIKA kuhakikisha masomo ya Sayansi,Hisabati na Teknolojia yanapewa kipaumbele katika ufundishwaji na kufanyiwa utafiti,serikali imekuja na mkakati wa kutoa motisha kwa wahadhiri katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda amebainisha hayo mkoani Singida wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa walimu wa Sayansi hisabati na kuongeza kuwa,wizara yake imeandaa mil 50 ikiwa ni kutekeleza mkakati huo kwa vitendo.
Prof.Mkenda alisema kuwa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetoa motisha ya sh. milioni 50 kwa wahadhiri kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanafundisha masomo ya Sayansi , Hisabati na Teknolojia, sanjali na kufanya utafiti na kuchapisha kwenye majarida mbalimbali ya kimataifa na watakaofanya vizuri watapata zawadi.
Aidha alisema kuwa hatua hiyo inaelenga kuzalisha tafiti nyingi za kisayansi ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali na kutoa fursa kwa wahadhiri hao kutambulika kimataifa na kujiingizia kipato.
Prof. Mkenda alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya mageuzi ya elimu nchini kwa kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kupitia mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini( SEQUIP) ili kuzalisha wanafunzi wengi wa sayansi ambao baadae watasaidia kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali.
"Wizara kupitia Programu ya Samia Extended imepanga kutoa ufadhili wa masomo ya sayansi kwenye nguvu za Atomic katika vyuo Vikuu nje ya nchi" alisema.
Alibainisha pia kwamba Serikali imejiandaa kikamilifu kutekeleza program hiyo kinachofanyika kwa sasa ni wanafunzi kuhamasishwa kusoma masomo hayo na kufanya vizuri ili kupata ufadhili kwenda nje ya nchi.
Alisema kuwa wizara imejipanga kuwafadhili vijana watakofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi, hisabati na teknolojia, kwa waliofanya vizuri watapata Fursa ya kwenda nje ya nchi kusoma kwamba serikali itagharamia kila kitu ili wakajifunze namna ya kutekengeneza atomiki mbalimbali,

No comments:
Post a Comment