MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO,MHE.ZAINABU KAWAWA ALIYESIMAMA AKISISITIZA JAMBO KABLA YA KUKABIDHI MSAADA KWA TIMU YA SOKA YA BAGAFRIENDS KULIA KWAKE NI KATIBU TAWALA WILAYA YA BAGAMOYO,KASILDA MGENI(VAZI LA PINKI)
DC AWAPIGA JEKI SEKTA YA MICHEZO,BAGAFRIENDS WALAMBA KITITA
NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
MKUU wa
Wilaya ya Bagamoyo Mh. Zainabu Kawawa katika kuunga mkono juhudi za kukuza
sekta ya michezo ametoa sapoti kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki tatu kwa
kikosi cha timu ya soka ya Bagafriends ambayo ni mabingwa wa Mkoa wa Pwani
katika michuano ya ligi daraja la tatu ambayo kwa sasa inajiandaa
na kivumbi cha ligi ya mabingwa wa mikoa ngazi ya Taifa inayotarajia kuazna
kutimua vumbi lake mwishoni mwa mwezi huu 2021.
Kawawa ametoa mchango huo wakati alipokutana na viongozi mbali
mbali wa mchezo wa soka wa Wilaya ya Bagamoyo,viongozi pamoja na wadau
wengine wa michezo lengo ikiwa ni kukutana kwa ajili ajili ya
kujadli na kupanga mikakati ambayo itasaidia timu hiyo iweze kufanya vizuri
sambamba na kuchangisha fedha ambazo zitasaidia wachezaji katika kipindi cha
ligi hiyo ngazi ya Taifa.
Pia Kawawa amewaomab wadau mbali mbali wa michezo katika Wilaya
ya Bgamoyo pamoja na Pwani kwa ujumla kushikamana kwa pamoja katika kuisaidia
kwa hali na mali timu hiyo ili iweze kutimiza malengo yake yakuweza kufanya
vizuri katika ligi hiyo na kupanda daraja katika msimu unaokuja.
“Hii ni timu yetu ya Bagafriends kwa hiyo mimi kaka mkuu wa
Wilaya ninawaomba wadau wa mchezo wa soka ndani ya Bgamoyo pamoja na Mkoa wa
ujumla tushikamane kwa pamoja kwa ajili ya kuipa sapoti ya kuisaidia michango
mbali mbali ili wachezaji ambao wanaunda timu hii waweze kucheza kwa molali
zaidi na kutuwakilisha vema katika michuano ya ngazi ya Taifa,”alifafanua
Kawawa.
Kadhalika aliwaasa viongozi wa mpira wa soka katika Wilaya ya
Bagamoyo kuweka mipango kabambe ya ambayo itaweza kufanikisha kupatika kwa ushindi
wa timu hiyo ya Bagafriends lengo ikiwa ni kufanya vizuri zaidi katika michuano
hiyo ya ngazi ya Taifa na kuongeza kuwa kwa sasa timu hiyo inatakiwa mahitaji
mbali mbali ya msingi ikiwemo vifaa, fedha, mipira pamoja mambo mengine.
Pia Mku huyo aliongeza kwamba katika kuhakikisha kwamab
sektya ya michezo inaendelea zaidi serikali ya Wilaya ya Bgamoyo itaendelea
kushirikiana bega kwa bega wadau tofauti katika kuhakikisha kwamba timu ya
bagafriends inaweza kufika mbali na kuibuka na ushindi katika kila mchezo lengo
ikiwa ni kuipeperusha vema Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani.
Aidha aliwataka wachezaji wote ambao wanaunda timu hiyo ya
Bagafriends kuwa na bidii katika michezo yote na kuwa na nidhamu ya mchezo
pindi wanapokuwa uwanjani na kuzingatia sheria zote 17 za mchezo wa soka na
kwamba ataendelea kuwapa sapoti mbali mbali kutoka kwake ili kuweza kutmiza
malengo amabyo wamejiwekea.
“Hii timu kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Mkoa wa Pwani
katika ngazi ya Taifa kwa hivyo hatuna budu wote kwa pamoja tukawa kitu
kimoja bila kujali timu imetokea sehemu gani lakini tutambue kwamba ndio
inauwakilisha Mkoa lakini mimi nina imani tukishikamana kwa pamoja tutaweza
kuleta mabadiliko zaidi katika Nyanja ya mchezo wa soko,”alisema Kawawa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo
Kasilda Mgeni aliwaomba wadau mbali mbali wa mchezo wa soka katika Wilaya
ya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuichangia timu
hiyo ya Bagafriends ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ya michuano
ya mabingwa ngazi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment