WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO KIBAHA WAKUBALI KUHAMIA ‘MAKAZI MAPYA’
NA
VICTOR MASANGU, KIBAHA
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristi Ndikilo amelazimika kuingilia
kati sakata la mgogoro wa siku nyingi, lililokuwa linawakabili wafanyabiashara
wadogo wadogo wa soko la Picha ya ndege Wilayani Kibaha waliogoma
kuondoka kupitisha mradi wa upanuzi wa barabara kuu ya Morogoro
Ndikilo
amewataka wafanyabisha wote wa picha ya ndege kuhama mara moja na kwenda katika
eneo maalumu ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya kuendeshe shughuli
mbalimbali za biashara kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa hali ya
sintofahamu na kuamua kwenda kusuluhisha jambo hilo akiwa ameambatana na kamati
ya ulinzi na usalama.
Aidha Mkuu
huyo aliongeza kuwa eneo hilo ambalo hapo awali walikuwa wafanyabiashara
wanafanyia shughuli zao lipo katika eneo la hifadhi ya barabara ya
morogoro hivyo ni hatarishi sana kwa usalama wa maisha yao ukizingatia na
magari mbali mbali yanapita karibu na eneo hilo.
“Kitu
kikubwa ambacho leo nimekuja na kamati yangu ya ulinzi na usalama ni kwa ajili
ya kuweza kujionea hali halisi pamoja na kujiridhishwa maana kumekuwepo na
mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakisemwa na wafanyabishara hawa lakini
nilishatuma timu yangu na imeniletea majibu kwa hivyo kitu kikubwa ni kuwaeleza
kuwa eneo hilo lipo katika hifadhi ya barabara na ni hatarishi sana kwa maisha
yetu” Alihadharisha.
Ndikilo
alisema kwamba, serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha
kwamba inawawekea mazingira rafiri ya kufanyia kazi wajasiriamali wote bila ya
kuwabagua na sio kwa nia ya kuwaonea na kwamba eneo jipya ambalo limetengwa kwa
ajili ya soko litakuwa la kudumu, lengo wafanyabishara waweze kufanya kazi zao
bila kusumbuliwa.
Kadhalika,
ndikilo aliwaonya baadhi ya wafanyabiashara ambao bado wanafanya shughuli zao
katika maeneo ya vichochoroni ambayo sio rasmi na kuwataka wote kuhakikisha
wanahamia katika soko hilo jipya ambalo litakuwa na miundombinu rafiki ambayo
itaweza kuwafanya kuendesha shughuli zao mbali mbali bila matatizo yoyote.
Aliziagiza,
mamlaka mbalimbali zinazohusika ikiwemo Dawasa, Tanesco pamoja na Tanrods,
kuhakikisha kwamba wanapeleka huduma katika eneo hilo la soko ikiwemo suala la
upatikanaji wa maji safi na salama, kuwepo kwa nishati ya umeme kwa bei ambayo
ni rafiki kutokana na eneo hilo la ni muhimu kwa wafanyabiashara.
Kwa Upande wake, Diwani wa kata ya picha ya ndege ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha, ameiomba serikali kuhakikisha inawaboreshea huduma ya miundombinu ya barabara na choo,na uwepo wa stendi, maji pamoja na umeme ili wafanyabiashara hao waweze kuendesha shughuli zao katika mazingira ambayo ni rafiki.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, (kushoto) akiwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege, (kulia),Mussa Ndomba wakielekea katika eneo la zamani la soko la picha ya ndege wakiligagua wakati wa ziara yake
ya kikazi kwa ajili kwenda kujionea eneoa la zamani pamoja na eneo jipya
lililotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara.
Kufuatia hamko na maelekezo hayo ya serikali ya Mkoa,wafanyabishara hao wamekubali kuhamia katika soko jipya la picha ya ndege licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kujipatia kipato zikiwemo huduma ya choo pamoja na baadhi yao kuuzia bidhaa zao katika maeneo ya vichochoroni,hata hivyo wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa jitihada zake za kusimamia maendeleo katika mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment