KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI,WANKYO NYIGESA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI
ASKARI POLISI PWANI ADAIWA
KUJINYONGA KWA KAMBA
NA VICTOR MASANGU, PWANI
ASKARI wa jeshi la Polisi aliyekuwa anafanya kazi katika
kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani namba E
6472 Yusuph Said mwenye umri wa miaka (52)
amekutwa amejinyonga hadi kufariki dunia katika
nyumba yake anayoijenga katika maeneo ya miembe saba, Kata ya
Kongowe Wilaya ya Kibaha.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambalo limetokea katika eneo la Miembe saba B kata ya Kongowe Wilayani
Kibaha ambapo alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni.
Kamanda Wankyo, alisema Yusuph alikua akitumikia katika kituo C,
anaishi Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo
anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.
YUSUPH SAID (52) ASKARI POLISI MWENYE NAMBA E 6472 ANAYEDAIWA KUJIUA KWA KUJINYONGA KIBAHA PWANI
Kamanda, alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo,
unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa
maziko zikiendelea.
Msaidizi wa balozi wa nyumba kumi, kwenye eneo hilo, Imelda
Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga
ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.
Imelda alisem,a alipofika alielewa na wazazi wa watoto waliokuwa
na karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya
nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na
walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na
walikimbia kwenda kutoa taarifa.
Wazazi hao, walipofika katika nyumba hiyo ambayo bado inajengwa
walimkuta askari huyo tayari ameshafariki ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa viongozi
na kumpigia msaidizi wa balozi wa nyumba kumi.
"Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na
baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua
kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikua na tofali
ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na
mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni" alisema
Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo
walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.


No comments:
Post a Comment