Na
Mwandishi wetu
MKUTANO mkuu wa Wanachama wa Klabu ya
waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro(MOROPC) imewapitisha wanachama wapya 20 na
kufanya idadi ya wanachama kufikia 100.
Mwenyekiti
wa Moropc,Bw.Nickson Mkilanya(picha) amewataja wanachama wapya hao ni Mhe.Bakar
Msulwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambaye
amepewa Uanachama wa Heshima kutoka na mchango wake mkubwa katika jamii.
Bw.Mkilanya
amewataja wanachama wapya mbani na mkuu wa Wilaya ni pamoja na Shua Nderaka,Peter Laurent,Sifuni
Mshana,Juma Kapalatu,Happines Mremi,Yusuph Ramadhan Kayanda na Elias Maganga.
Wengine Mkilanya amewataja ni Remmy
Yasinti,Isdory mtunda,Rifati Jumanne,Fatuma Mtemangani,Costancia Michael,Peter Mtulia,Kalokola
Epimacus Apolonary,Josephine Malango, Omar Hussein na Farida Mangube.
Hata hivyo,Bw.Mkilanya amesema
yapo maombi mengine ya wanachama watatangazwa hivi karibuni baada ya
kujiridhisha na rekodi zao na haiba walizonazo katika jamii.
No comments:
Post a Comment