Breaking News

Sep 12, 2020

JICHO LANGU:Tasnia ya habari Moro yang'ara medani za kisiasa 2020

"KILA zama na vitabu vyake",unaweza kunukuu msemo huu kutoka kwa wanazuoni na wabobezi wa Semi na Nahau kwa lengo tu la kuangalia dhana nzima ya mchakato wa siasa ulivyoanza au toka kipenga kilipopulizwa na mamlaka.
Mwaka huu 2020,ambao ni mwaka wa uchaguzi wakupata madiwani,wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeweza kushuhudia mchakato wa kada mbalimbali wakiwemo wanataaluma mbalimbali wameonekana kujitokeza kwa kutia nia ya kugombea nafasi mbalimbali za kiasiasa ikiwemo ubunge na udiwani ambapo baadhi yao waliomba likizo isiyokuwa na mafao kwa mabosi wao ili kufanikisha malengo waliyakusudia.
Taaluma ya habari kama ilivyo kwa kada nyingine nao hawakubaki nyuma nao wamejitosa kuwania nafasi ama ya ubunge au udiwani katika kata na majimbo yakiyowapendeza kutangaza nia.
Mkoa wa Morogoro kama ilivyo kwa mikoa mingine kuna idadi kubwa ya waandishi wa habari ambao wanafanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya watu binafsi,taasisi za dini na serikali pia, baadhi yao walitia nia ya kugombea nafasi hizo muhimu za uwakilishi wa wananchi katika ngazi za uamuzi.
Mchakato ulianzia kwenye vyama vyao vya siasa ambako waliomba ridhaa kwa wajumbe ili chama kiweze kuwapa kibali cha  kupeperusha bendera ili mwisho wa siku wapate ushindi katika uwanja  sawa wa ushindani wa siasa za vyama vingi kama ilivyo kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Wapo waliotia nia kwenye viti maalum ubunge na udiwani,wapo walitia nia kwenye ubunge wa majimbo na udiwani kwenye ngazi ya kata,kila mmoja alijinadi na kung’arisha nyota yake kwa wajumbe kwa kuomba kura.
Waliotia nia kwa wanahabari wa Morogoro ambao baadhi yao wamefanikiwa kupenya kwenye kapu la vyama vyao huku wengine wakijipanga tena kwa kipindi kingine kutokana na wajumbe kuwapa muda zaidi wa kujiandaa,wajumbe hakika nao walikuwa na yao ya moyoni!.
Wanatasnia hao ambao leo ninawaita, Nyota ya tasnia ya habari yang’ara 2020 ndani ya  Morogoro waliojitokeza ni Salum Mkolwe (Ubunge CCM-Jimbo Morogoro mjini),Idda Francis Mushi (Ubunge jimbo CCM-Moshi vijijini),Calvin Gwabala (Ubunge CCM jimbo-Morogoro mjini),Josephine Mallango (Udiwani viti maalum CCM),Latifa Ganzel (Udiwani viti maalum CCM),Loveness Nyawili (Udiwani viti maalum CCM),James Mkisi(Udiwani CCM Kata),Samuel Msuya (Udiwani Kata CCM-Mbuyuni),Ramadhan Libenanga(Udiwani Kata uwanja wa taifa-CCM), Devotha Minja (Ubunge Jimbo CHADEMA-Morogoro mjini) na Victor Makinda Udiwani CCM- Kisawasawa,Kilombero)
Nyota hao wa tasnia ya habari waliweza kutimia haki yao ya kidemokasia ndani ya vyama vyao kabla ya kupewa kibali na tume ya uchaguzi.hata hivyo baadhi yao wajumbe kutoka kwenye vyama vyao wamewapa muda zaidi wa kujiandaa katika kipindi kingine baada ya  kuwa kura walizopata katika nafasi walizowania hazikutosha.Sisi kwetu wote ni mashujaa na leo tunawaita kuwa ni nyota wa tasnia ya habari katika medani ya siasa 2020.Tukutane tena kwa mara nyingine kwenye jicho langu!!!!!  


 kwa maoni na ushauri wasiliana nasi kwa namba

0658683186: E-mail hafigwa@yahoo.com

No comments:

Post a Comment