Lionel Messi aliichezea kwa mara ya kwanza Barcelona tangu jaribio lake la kutaka kuondoka kugonga mwamba akishiriki katika mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Gimnastic de Tarragona.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika klabu hiyo mwezi Agosti lakini akaamua kusalia kwasababu hakuna klabu ingeweza kutoa fedha za kifungu cha sheria cha kumuondoa katika klabu hiyo.
Messi alianza katika mechi hiyo ambapo Barcelona ilijipatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya klabu ya ligi ya daraja la tatu Nastic baada ya klabu hiyo kuthibitisha kwamba atasalia kama nahodha wake.
No comments:
Post a Comment