Breaking News

Sep 12, 2020

DC Msulwa Ahimiza wananchi kudumisha amani kipindi cha kampeni uchaguzi oktoba.


Na Mwandishi wetu

MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Bw.Bakar Msulwa amewaasa wanasiasa na wakazi wa Wilaya ya Morogoro kudumisha amani hasa katika kipindi cha kampeni kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Raisi.

Rai hiyo ameitoa wakati akiongea na wakazi wa Morogoro kuhusu dhana ya demokrasia na uchaguzi,kwamba uwepo wa kampeni haina maana ya kwamba watu kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali na kuhatarisha amani na utulivu uliopo.

Aidha,Aliasa kwamba serikali ipo macho katika kuhakikisha ya kuwa amani na utulivu inaendelea kudumu na kwamba hivyo kila mdau wa amani anapaswa kuzingatia misingi iliyoasisiwa na viongozi wa taifa ya kuheshima sheria bila ya kushawishiwa kuleta uvunjifu wa  amani.

Alisema ya kuwa kila mwanasiasa hapa nchini awe kutoka chama cha mapinduzi au chama cha upinzani 

wajibu wao ni kulinda na kudumisha amani katika kipindi chote cha kampeni ili taifa liendelee kuwa na mshikamano na upendo huku jamii ikiheshimu na kufuata sheria.

wakati huo huo,Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro,MOROPC imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw.Bakar Msulwa kwa ushirikiano anaoutoa kwa waandishi wa habari wa Morogoro.

Bw.Msulwa ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa habari hivi karibuni ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kushika wadhifa wa ukuu wa Wilaya baada ya Bi.Regina Chonjo aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo kustaafu.

Katibu Mtendaji wa Morogoro Press Club,Bi Lilian Lucas katika mahojiano na Moropc blog amesema ya kuwa Bw.Msulwa toka alipofika Morogoro amekuwa na ushirikiano mkubwa na waandishi wa habari jambo ambalo linazidi kuimarisha mahusiano mema kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari waliopo Morogoro.

Bi.Lilian amesema hatua hiyo anaamini inafungua ukurasa mwa wadau wengine wa habari ambao wamekuwa wazito kwa wanahabari katika utoaji wa taarifa kubadili fukra zao ili dhana ya haki ya kupata na kutoa habari zenye tija kwa taifa iweze kuweze kutekelezwa kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment