Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba. |
Halmashauri ya Manispaa ambayo ninaongozwa na Mkurugenzi wake
Mwanamke shupavu, Sheilla Lukuba ina Katika
mfumo wa Utendaji, kwa kuwa na Idara
kumi na tatu na Vitengo sita vinavyowajibika
moja kwa moja kwa Mkurugenzi. Idara kumi na tatu za Halmashauri ni pamoja na Utawala na Utumishi,Fedha na Uongozi,Afya,Elimu
Msingi,Elimu Sekondari,Mipangomiji na Ardhi,Maji,Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Mifugo
na Uvuvi,Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika,Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji,Usafi
na Mazingira,Ujenzi na Zimamoto
Huku kukiwa
na vitengo vitano
ambavyo ni-,Sheria,Ukaguzi wa Ndani,Ugavi,Uchaguzi,Ufugaji
Nyuki,Teknologia,Habari, Mawasiliano na Uhusiano Hivyo Manispaa ya Morogoro
katika mfumo wake wa utawala huundwa kwa njia ya Kamati ambazo ndio injini za uendeshaji wa kazi zake,Kamati hizo ni,Kamati
ya Fedha na Uongozi, Kamati ya Huduma za Uchumi, Elimu na Afya,Kamati ya
Mipangomiji na Mazingira,Kamati ya kudhibiti Ukimwi na Kamati ya Maadili.
Kwa
kuzingatia Dira ya Maendeleo ya 2025, Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini Tanzania (MKUKUTA) II na Malengo ya Millenia ili kutoa huduma bora kwa
jamii.
Katika jicho
la Moropc blog leo tunaangazia sekta ya elimu ilivyowekewa msingi kwa wananchi
ili waweze kunufaika.Elimu
ya Msingi:Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina jumla ya
shule 85 za Msingi, kati ya hizo shule 62 ni za Serikali na shule 25 zisizo za
Serikali. Jumla ya wanafunzi walio katika shule za msingi za Serikali ni 50,448
kati yao wavulana ni 24,891 na wasichana ni 25,557.
Kadhalika Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA) Mpango huu unasimamia
watoto wanaostahili kwenda shule na hawakupata fursa .Watoto hawa
wanaandikishwa katika shule ya Msingi.MEMKWA ina jumla ya Wanafunzi 251, kati
yao Wavulana ni 146 na wasichana ni 105.
MUKEJA: Huu ni mpango kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii,kundi hili
lina jumla ya Washiriki 233.Katika mpango huu wanakisomo hupata mbinu za
kujiajiri kama ushonaji,Useketaji,Ususi,Ufinyanzi,Ufumaji,Ufugaji,Kilimo na
bustani,ufundi cherehani na utunzaji wa Mazingira.Pia kuna wanakisomo chenye
manufaa KCM Washiriki 157,Wanakisomo cha kujiendeleza washiriki 76.
Vituo vya Ufundi Stadi:Manispaa ina vituo viwili (2) vya Ufundi Stadi vyenye wanafunzi 131, wakiwemo wasichana 79 na wavulana 52 waliomaliza Elimu ya Msingi na ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na Elimu ya Sekondari. Vituo hivi ni Msamvu na Luhungo ambavyo hufundisha Useremala na Sayansi Kimu. Wanafunzi hawa baada ya kumaliza mafunzo haya hujiajiri au kuajiriwa katika fani walizosomea.
No comments:
Post a Comment