Bwa.AbdulazizAbood Mgombea nafasi ya Ubunge, Jimbo la Morogoro Mjini. |
Na Ashton Balaigwa,MOROGORO
MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge Jimbo la
Morogoro mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulaziz Abood
,amesema anapaswa kuchachuliwa kwa mara nyingine kwakuwa amefanikiwa kuibana
Serikali na kupelekea Rais Dk John Magufuli kutoa fedha zaidi ya Shilingi
bilioni 185 kwa ajili ya kuhakikisha kero ya
maji inamalizika Manispaa ya Morogoro.
Kutokana na hali hiyo ameaomba
wananchi wa jimbo hilo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi
Oktoba 28, mwaka huu(2020) kuwachagua wagombea waliosimamishwa na chama
hicho kuanzia ngazi ya Rais, Ubunge na Madiwani ili waendelee kuwaletea
maendeleo endelevu.
Kwa kipindi kirefu sasa wakazi wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji katika maeneo yao.
Abood , alisema hayo wakati
wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi ya chama hicho wilaya
ya Morogoro mjini kwenye uwanja wa Shujaa uliopo kata ya Mji Mpya ,
Manispaa ya Morogoro.
Katika uzinduzi huo mgeni rasmi
alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Innocent
Kalogeris ambaye pia ni mbunge mteule wa Jimbo la Morogoro
Kusini kupita chama hicho.
“ Nimekuja kwenu kuomba mnipe tena ridhaa
yenu ya kuwaongoza miaka mingine mitano ili niweze kuendelea na kazi
zilizobaki na kazi kubwa ambayo nina ijua ni kero kubwa katika mji
wa Morogoro ni suala la maji ambalo tayari serikali imeshaanza kutoa
hela” alisema Abood.
Alisema kuwa katika kuondoa kero
hiyo,tayari Rais Dk Magufuli,ameweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 185
kwa ajili ya mradi huo, kwamba, wakati wowote
utaanza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kata za
Bigwa, Mkundi , Lukobe , Mindu na Kingolwira.
Alisema kwa kipindi cha
miaka kumi ya ubunge amekuwa si mbunge wa maneno maneno bali ni
wa vitendo zaidi kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu ya
wananchi ,na kwamba chini ya Serikali ya iliyopo madarakani
Maniapaa ya Morogoro imesonga mbele kimaendeleo .
Hata hivyo, alisema chini ya
Serikali imeweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika
Manispaa ya Morogoro ikiwa na uboreshaji wa huduma za
afya , elimu na miundombinu ya barabara ,umeme na huduma za kijamii
ikiwemo utoaji wa mikopo kwa wanawake , vijana na watu wenye ulemavu.
Hivyo, alitumia fursa hiyo
kuwaomba wananchi wa Manispaa hiyo wenye
sifa za kupiga kura kujitokeza siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka
huu na kumpigiaakura zote mgombea urais wa CCM , Dk John Magufuli .
Jimbo la Morogoro Mjini lina jumla ya kata 29,ambapo kwa upande wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wameweza kuweka wagombea wote baada ya Tume ya Uchaguzi kuwapitisha kugombea nafasi hizo.
No comments:
Post a Comment