Na Ashton
Balaigwa,MOROGORO
SERIKALI kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Imeanza
mkakati wa kulifufua zao la korosho katika Mkoa wa Morogoro ili kulifanya zao
hilo kuwa moja ya zao la biashara litakalosaidia kukuza uchumi wa mkoa
huo.
Kupitia
mkakati huo TARI Naliendelea iliyopo mkoani Mtwara imeanza sasa
kutoa mafunzo kwa wakulima wa zao hilo la korosho kwa mkoa wa Morogoro ili
kuwapatia mbinu bora za ulishaji wa zao hilo la korosho .
Hivi
karibuni wakulima wa zao la korosho wamekuwa wakiendesha shughuli zao za kilimo
katika mfumo wa mazoea badala ya kuendesha kibiashara.
Mratibu wa zao la
korosho kutoka TARI Dk Geradina Mzena,alisema lengo kuu ni kutaka kumuondoa
mkulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuanza sasa kulima kilimo cha
biashara kwa kuwajengea uwezo wakulima
wa zao hilopamoja na maafisa ugani.
Dk Mzena
alisema kuwa ili kwakua Morogoro ina wakulima wapya na lengo ni kukifanya
kilimo hicho cha korosho kuwa cha kibiashara ni lazima kuwapatia mafunzo ya
namna ya kutunza zao hilo la korosho pamoja na changamoto mbalimbali za kilimo
hicho.
“ Tunatambua
Hii ni mikoa mipya yenye wakulima wa zao la korosho hivyo tumeona kuwa
tuwapatia mafunzo ya kilimo bora cha zao la korosho ili waweze
kulima kilimo cha kibiashara”Alisema Dk Mzena.
Mmoja wa
wakulima wa zao hilo,Neema Marwa kutoka wilayani Mvomero,alisema ameamua kuanza
kulima kilimo hicho cha korosho,baada ya kuhamasika na kuwa na uwakika wa soko
lake ukilinganisha na kilimo cha mazao mengine ya biashara.
Naye Martini
Joseph mkazi wa Morogoro vijijini,alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuamua
kutoa mafunzo ya kilimo hicho cha korosho ambacho kimekuwa na gharama nafuu na
chenye kuleta tija na mafanikio kwa haraka tofauti na kilimo kingine.
Akifungua
mafunzo hayo,Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na
Uzalishaji,Rosaria Rwegesira,alisema kuwa kwa miaka ya nyuma mkoa wa Morogoro
ilikuwa miongoni mwa mikoa inayolima zao hilo lakini kutokana na kutokuwa na
soko la uwakika wakulima walikata tamaa.
Alisema
kutokana na hamasa katika miaka ya hivi karibuni wakulima wameamua kuanzisha kilimo
hicho ambapo mwaka 2018 zilipatikana jumla ya tani 63 na mwaka 2019
ziliongezeka na kufikia tani 183 hivyo kupitia mafunzo hayo uzalishaji huo
utaendelea kuongezeka na kuwa miongoni mwa mikoa ambayo
inazalizalisha korosho.
No comments:
Post a Comment