Wanasayansi 300 wazindua ripoti ya ulinzi wa ozoni
Kila mwaka ifikapo septemba 16 duniani huadhimisha siku ya kimataifa ya kulinda tabaka la ozone Juhudi za kimataifa za kulinda tabaka hilo ambalo ni ngao inayolinda dunia kutokana na miale hatari ya jua zimetajwa kama mafanikio ambayo yamefaulu kuzuia kuharibiwa zaidi kwa tabaka hilo.
Ripoti mpya iliyoandaliwa na karibu
wanasayansi 300 imezinduliwa leo katika kuadhimisha siku hii na kusema
makubaliano ya Montreal yamefanikiwa kulilinda tabaka la ozone
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inaonyesha kuwa kati ya vitu
vinavyochangia kuharibika kwa tabaka hilo la ozone ni pamoja na gesi chafu huku
makubaliono ya Montreal yakichangia manufaa makubwa kwa kupunguza mabadiliko ya
hali ya hewa.
Ripoti hiyo iliyochapishwa na shirika la hali ya hewa
duniani WMO kwa ushirikiano na shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP inasema
kuwa suala muhimu kwa sasa ni kulinda tabaka la ozone.
kwa siku zijazo na kuelewa zaidi athari za mabadiliko ya hali ya hewa Ripoti hiyo inaongeza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatarajiwa kuwa na athari zaidi kwa tabaka la ozone kwa miaka kadha inayokuja huku shughuli za kibinadamu na gesi inayochafua mazingira vikitajwa kuchangia hali hii(chanzo habari za UN)Kauli mbiu ya mwaka huu 2020,Kulinda tabaka la ozoni, utawala na utekelezaji ndio nguzo.
No comments:
Post a Comment