Na Thadei Hafigwa
KATIBU wa Umoja wa Machifu Tanzania, Chifu Aron Nyamironda wa Pili kutoka mkoani Mwanza, amesema kuwa uamuzi wa serikali kwa kuwashirikisha Machifu katika tamasha la utamaduni i na kutambua mchango wao katika kurejesha, kuenzi na kuhifadhi mila na utamaduni wa Mtanzania.
Chifu Nyamironda amebainisha hayo kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla ya kufunga tamasha hilo la nne la kitaifa lililofanyika mkoani Morogoro,aliongeza kuwa moja ya majukumu ya Machifu ni kuhakikisha utamaduni wa Mtanzania unadumishwa na kurithishwa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Chifu Nyamironda alisema wamefarijika kuona mwamko mkubwa wa vijana waliojitokeza kushiriki na kushuhudia tamasha hilo, jambo ambalo linaonesha bado kuna nafasi ya kuendeleza mila, desturi na utambulisho wa makabila mbalimbali nchini.
“Miongoni mwa majukumu yetu ni kuikumbusha jamii, kwa vitendo, historia na asili ya Mtanzania, alikotoka na anakokwenda, lakini pia kushiriki katika utunzaji wa maeneo na vitu vya kihistoria kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema.
Awali, akitoa salamu za Mkoa wa Morogoro, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Sebastian Waryuba, alisisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kutunza amani na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha mshikamano na utulivu wa nchi.
Ramadhan Divunyagale,Mwenyekiti wa Mila na Desturi Mkoa wa Morogoro(SHIWAMILA) amesema kuwa wazee wa Mkoa wa Morogoro watahakikisha ya kuwa maadili kwa vijana na


No comments:
Post a Comment