PSSSF INAVYOHAMASISHA TIJA KAZINI: TRAFIKI AJINYAKULIA KITITA KILELE CHA WIKI YA MTEJA
Askari wa Usalama Barabarani, Bw. Ashraf Shaaban, akikabidhiwa kitita cha Sh1m/- taslim na PSSSF Kanda ya Kinondoni Dar es Salaam leo, kama motisha kwa kuonesha tija katika eneo lake la kazi. PSSSF imetoa hamasa hiyo kwa trafiki huyo katika kilele cha huduma kwa mteja.
Na Mwandishi wetu
Katika kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja,mfuko wa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishk wa Umma(PSSSF) imeweka rekodi ya kipekee kwa kutoa motisha kwa askari wa usalama Barabara,Ashraf Shaaban kitita Cha shilingi milioni Moja(1,000,000).
Ifahamike kuwa,utoaji wa motisha kazini huongeza ari kwa wafanyakazi na kuleta tija katika sehemu ya kazi.
Katika kudhitisha hali hiyo,wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Kanda ya Kinondoni, Dar es Salaam, wamemtunuku, Askari wa Usalama Barabarani,,Ashraf Shaaban, fedha taslim, kiasi cha Shilingi 1,000,000.00 Milioni Moja) taslim,
kutokana na kuipenda kazi yake, akionesha bidii katika eneo lake la kazi, lugha nzuri kwa watumiaji wa barabara na ubunifu akiwa anaongoza magari na kuwasaidia raia waenda kwa miguu.
*PSSSF daima iko na Wafanyakazi na Wastaafu wote wa umma, JANA, LEO NA KESHO.
No comments:
Post a Comment