Breaking News

Jun 8, 2021

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA KUANZA NCHI NZIMA


UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA KUANZA NCHI NZIMA
 

Na.Victor Masangu,Bagamoyo

NAIBU katibu mkuu Ofisi ya Rais Gerad Mweli amewagiza maafisa elimu wa mikoa pamoja na wakurugenzi nchi nzima kuhakikisha kwamba wanaanza mara moja ujenzi wa miradi ya madarasa kwani fedha zake zimeshatolewa na serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

Mweli alisema hayo wakati wa kufunga rasmi mafunzo  ya kuwajengea uwezo katika suala la uthibiti ubora wa elimu kwa maafisa elimu wa mkoa nchi nzima,maafisa taaluma wa mikoa pamoja na Maafisa elimu msingi wa halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa Adem Wilayani Bagamoyo

Aidha, aliwataka kuhakikisha kwamba wanakwenda kuyatumia vizuri mafunzo hayo waliyopatiwa kwa ajili ya kuthibiti ubora wa elimu na kuweka mikakati mathubuti ambayo itaweza kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini.

Naibu katibu mkuu huyu alisema lengo la serikali ni kuboreha sekta ya elimu hapa nchini hivyo maafisa elimu hao pamoja na Maafisa taaluma wanapaswa kusimamia ipasavyo fedha zote ambazo zinatolewa na serikali katika kutekeleza miradi mbali.mbali ya elimu.

Aliongeza kuwa anasikitishwa kuona hadi sasa Kuna baadhi ya halmashauri nchini zimepatiwa fedha lakini zimeshindwa kuanza kabisa ujenzi wa madarasa ambapo ameahidi kulivalia njuga suala Hilo.

'Kwa kweli katika jambo hili siwezi kumvumilia mtu yoyote hata tunatakiwa tufanye kazi maana Mimi nimepokea mezani kwangu halmashauri zipatazo ,60 serikali imezipatia fedha lakini cha kushangaza bado haziaanza kabisa ujenzi wa madarasa kwa kweli hili jambo siwezi kulifumbia macho,'alisema

Kadhalika, aliwakumbusha maafisa elimu hao kutumiza wajibu wao ipasavyo na kuwema mipango madhubuti katika kuboresha miundonbinu ya madarasa kwani Kuna maeneo mengine madarasa bado ni chakavu.

Katika hatua nyingine aliupongeza uongozi wa Adem kwa kuweza kutoa mafunzo hayo ya siku nne kwa maafisa elimu hao ambayo yatawasaidia katika kuongeza Chachu zaidi katika suala la usimamizi wa elimu hapa nchini.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Adem Dr.Siston Mgullah amebainisha kuwa lengi kubwa la kufanyika kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maafisa elimu hao katika suala zima la uthibiti ubora wa elimu.

Pia aliongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yamewashirikisha jumla ya washiriki wapatao 232 yataweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya elimu kutoka na mada mbali.mbali ambazo zimetolewa hivyo ana Imani maafisa elimu hao wataweza kuleta matokeo chanya.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Adem itaendelea kushirikiana na serikali bega kwa bega katika kuwapatia ujuzi wa Mara kwa Mara maafisa elimu wote katika ngazi mbali mbali hapa nchini lengo ikiwa ni kusaidia kuboresha elimu.

 Aliiomba serikali kuwapa kibali cha kwenda kutembelea katika shule mbali mbali ili kujionea mafanikio ambayo yametokana na mafunzo hayo na kwamba lengo lao kubwa ni kuona kunakuwa na mabadiliko chanya katika elimu.

 

 

No comments:

Post a Comment