MKUU WA MKOA WA MOROGORO,MARTNE SHIGELA
RC SHIGELA ATEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA SAMIA
Na Severin Blasio,Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela amepiga marufuku
halmashauri ya Manispaa Morogoro kutumia jeshi la akiba`mgambo`katika
ukusanyaji wa mapato badala yake watumike kulinda majengo.
Shigela ametoa agizo hilo juzi ikiwa ni siku chache
Rais Samia Suluhu Hassani kutengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya
Morogoro Bakari Msulwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheila Lukuba kwa
tuhuma za askari hao kuwapiga wafanyabiashara wa mbogamboga wakidaiwa kufanya
biashara kinyume cha sheria.
“Kuanzia muda huu naagiza wakurugenzi wote kuwa sitaki kusikia
operesheni ya kutumia mgambo kuwabughudhi wafanyabiashara ndani ya
mkoa huu.
“Kama mnawahitaji askari hao,watumie katika kulinda majengo yenu
,na siyo kuwatumia katika ukusanyaji wa kodi’Alisema Shigela.
Aidha, Shigela ametoa agizo la kupunguza tozo mbalimbali katika
soko la Kingalu zikiwemo za vizimba,vioski,wauza mitumba huku akifuta tozo za
boda boda na bajaj kwa lengo la kuwavutia wafanya biashara ambao walikimbia
soko hilo na baadhi yao kuanza kupanga bidhaa kando ya barabara.
Akizungumza na wafanyabiashara na machinga Shigela alisema
ametoa agizo hilo ili kupunguza masoko holela ambayo yamekuwa yakijitokeza
katika manispaa hiyo na hivyo kuathiri biashara zilizopo kwenye soko hilo ikiwa
ni pamoja na kupunguza mapato ya halmashauri.
Kwa mjibu wa Shigela tozo hizo zimepungua kutoka shilingi 20,000
hadi shilingi 10.000 kwenye vizimba,shilingi 200,000 hadi shilingi
50,000,fremu za juu ,shilingi 300,000 hadi shilingi 100,000 frem za chini na
shilingi 100,000 hadi 30,000 kwa wauza mitumba.
Shigela alisema utaratibu huo utaanza Julai mosi mwaka huu
na utadumu kwa muda wa miaka miwili jambo ambalo wafanyabishara hao
wameridhia.
Awali, mwenyekiti wa soko la Kingalu, Halid Mkunyagale alimwambia
mkuu wa mkoa huyo, kuwa wafanyabiashara wa soko hilo wana kero ya
masoko holela,tozo za gharama ya pango,maji na kukatwa kwa umeme.
Akijibu kero hizo, pamoja na mambo mengine,meneja wa soko hilo, Mwajui Sanga, alikiri kuwepo kwa kero hizo akidai tozo hizo zimepangwa kwa ajili
ya kusaidia kutoa huduma mbalimbali kama vile kampuni inayofanya usafi
na kulipia ankra za maji.
Hata hivyo, Meya wa manispaa hiyo, Pascal Kihanga amekubali agizo
la mkuu wa mkoa la kupunguza tozo za pango ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu
mzuri w kuhakiisha wafanyabiashara wote watakaohamia hapo wanapata nafasi
Soko la Kingalu toka lifunguliwe mwaka huu limekuwa na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo ukilitimba wa wafanyabiashara
kushindwa kupata sehemu ya kuuzia na kupelekea baadhi yao kupanga bidhaa zao
kando ya barabara.
No comments:
Post a Comment