Breaking News

Jun 19, 2021

TUME YA UCHAGUZI KUONDOA DOSARI ZILIZOJITOKEZA WAKATI WA UCHAGUZI

 TUME YA UCHAGUZI KUONDOA DOSARI ZILIZOJITOKEZA WAKATI WA UCHAGUZI

Lilian Lucas, Morogoro.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imedhamilia kumaliza na kuondoa  changamoto  mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika chaguzi zilizopita ambazo zilisababisha malalamiko kwa vyama vya siasa pamoja na wadau wengine na kupelekea uchaguzi kuonekana na dosari.

Hayo yalisemwa na mjumbe wa tume ya  taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Mary Longway alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi  na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi  ngazi ya jimbo na kata unaotarajiwa kufanyika julai 18 mwaka huu .

Alisema kuwa uchaguzi huo  mdogo  wa ubunge  utafanyika katika   jimbo la kondeanzibar  na  udiwani katika kata za ndirgish halmashauri ya wilaya ya kiteto, Mbagala kuu  halmashauri ya manispaa ya temeke , mchemo halmashauri ya wilaya ya Newala, mitesa halmashauri ya wilaya ya Masasi, chona halmashauri ya wilaya ya ushetu na Gare halmashauri ya wilaya ya Lushoto.

 Aidha, Jaji mstaafu Longway, alisema kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuisha  hatua na taratibu mbalimbali  ambazo ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa mzuri na wenye ufanisi  na hivyo kusaidia kupunguza kama sio kumaliza kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

Mjumbe huyo aliwataka washiriki wote wa mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia maelekezo watakayopewa na Tume ili waweze kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni badala ya kunya kazi kwa mazoea.

Alisema pia mambo muhimu ya kuzingatia  ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi  kwa kuzingatia katiba ya nchi, sheria za uchaguzi na kanuni zake , maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na tume.

Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi  jimbo  jimbo la Lulindi  ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi  Changwa mkwazu  aliwataka wagombea  wa vyama vya siasa kufuata maelekezo wanayopewa ili kusijekuwa na migogoro isiyo ya lazima wakati wanajua kabisa kuwa zipo taratibu za kufuata kama kuna jambo lolote limetokea  katika zoezi zima la uchaguzi.

Aidha, aliwaomba pia wanasiasa kule ambako uchaguzi unafanyika kufanya kampeni na uchaguzi wenye amani  na kuzingatia sheria walizoelekezwa na Tume.

No comments:

Post a Comment