Mkuu wa mpya wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Ahmed Abas akiwa anaapa mbele
ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge hayupo pichani wakati wa hafla hiyo.
RC
KUNENGE AWAFUNDA ‘MA-DC’ WA MKOA WA PWANI
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa
Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge amewaagiza wakuu wapya wa wilaya
waliochaguliwa hivi karibuni kuhakikisha kwamba wanatimiza majukumu yao
ipasavyo ikiwemo kulivalia njuga suala la kukomesha na kutatua suala la
migogoro ya ardhi sambamba na kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya
maendeleo kwa kuzingatai sheria na taratibu bila ya kufanya uonevu
wowote kwa wananchi.
Kauli hiyo, ameitoa wakati wa hafla fupi ya kuwapisha
wakuu wapya wa wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani ambao
wameteuliwa hivi karibuni na Rais wa awamu ya sita
Samia Suluhu Hassan kutoka, Wilaya za Mkuranga,
Kisarawe, pamoja na Kibiti na kuwataka kuweka mipango madhubuti ya
kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.
Pia, Kunenge amewasisitiza
wakuu hao wa Wilaya kusimamia sheria asiwepo mtu wa kupendelewa wala
atakayeonewa.
Aliwataka wakazi wa mkoa huo kuheshimu sheria huku akionya wenye
tabia ya kuvamia maeneo na kuyauza kuacha tabia hiyo.
" Baadhi ya migogoro ipo katika maeneo ambayo yana
hatimiliki za ardhi, kama shamba utaratibu upo utafuatwa na mamlaka
zinazohusika" alisema.
Mkuu huyo pia aliwawataka wakuu hao wa wilaya kutatua kero
za wananchi ambazo zipo ndani ya uwezo wao na zilizo nje wahakikishe
wanazifahamu kabla ya kuzifikisha mamlaka za juu.
"Kama kila mmoja atasimamia majukumu anayotakiwa hakutakuwa
na kero kwa wananchi siamini katika uongozi wa mtu mmoja tushirikiane na kila
mmoja awe tayari kujifunza" alisema.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka kushirikiana na Halmashauri kuongeza
mapato na kusimamia miradi ikamilike kwa wakati na kwamba kila
mmoja asimamia uainishaji wa maeneo ya uwekezaji lakini pia maboresho ya
madaftari ya makazi.
Kwa upande wake, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson
Saimoni almaarufu ‘niki wa Pili’ amesema kuwa atatekeleza maelekezo na
maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa na kwamba lengo lake kubwa
ni kutumia maarifa aliyonayo katika kuwaletea mabadiliko chanya wananchi
pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbali mbali zilizopo katika sekta
tofauti.
Kadhalika Mkuu huyo alisema pamoja na nafasi aliyopewa
mchango wake katika sanaa utaendelea kuwepo katika ajenda za kitaifa, Mkoa na
Wilaya.
Naye, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri
amemshukuru Rais kwa kumumini tena na kuahidi kushirikiana bega kwa began
a wananchi wake katika kutatua kero na kwamba atatumia fursa ya viwanda
vilivyopo katika kukuza uchumi na kuwapatia fursa ya ajira vijana ili kuweza
kuleta chachu ya maendeleo na kuondokana na wimbi la umasikini.
Sara Msafiri, aliahidi kutekeleza maagizo
ya mkuu wa Mkoa huku akisema ataanza kwa kukaa na wananchi kwenye maeneo ya
migogoro kuitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment