Msigwa:Vyombo vya Habari, waandishi wa habari vyatakiwa kuwa na mikakati ya kuvutia wawekezeji kwenye tasnia
Na.Lilian Lucas,DODOMA
Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amevitaka vyombo vya habari na waandishi wa habari nchi, kuwa na mkakati wa kuvutia wawekezaji katika tasnia hiyo, ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya uchumi kwa waandishi wa habari.
Alisema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania jijini Dodoma.
Msigwa alisema kama vyombo vya Habari ni lazima kuja na mkakati wa namna ya kuvutia wawekezaji kwenye sekta ya habari, na kwamba tasnia haiwezi ikawa mahali pa kuungaunga.
"Utakuta mwanahabari anajikusanyakusanya anapata fedha ananunua kebo(cable), ananunua kamera tayari anakuwa na chombo cha habari,kwangu Mimi naona haijengi kunatakiwa kuwa na Uwekezaji wenye tija, "alisema.
Msigwa ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya habari maelezo alisema uwekezaji katika tasnia ya habari ukiwa mkubwa unaweza kutatua changamoto ya uchumi wa vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania Salome Kitomaryi akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la kwanza, kupitia hali ya uchechemuzi ya uhuru wa kujieleza kwa miaka 30 ya taasisi ya Misa .Alisema ili kuwavutia wawekezaji katika tasnia ya habari ni lazima wanahari wenyewe kuonyesha umakini katika taaluma yao.
Pia Msigwa amezitaka taasisi zinazohusika na waandishi wa habari ikiwemo Misa Tanzania , kutoa mafunzo hususani kwa waandishi wa habari vijana ili kuwarithisha utamaduni mwema wa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Musa Tanzania Salome Kitomari alisema uchumi wa wanahabari wengi wana hali ngumu kimaisha, hawana mikataba, Bima za Afya na stahiki zingine za kisheria ikiwemo michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
"Niwaambie hali hii inaathari kubwa kwenye mchakato wa habari kwa kuwa kunatoa mwaya wa rushwa kwa sababu siku zote tumbo lenye njaa haliwezeshi ubongo kufikiria vyema,"alisema Salome.
Salome alitumia fulsa hiyo kuipongeza Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua mbalimbali zilizowezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuondoa vikwazo vingi katika sekta hiyo.
Alisema Misa ni taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika,ambapo ina matawi kwenye nchi za Angola,Botswana, Zambia , Malawi, Lesotho, Msumbiji na ambapo tawi la Misa Tanzania ilianzishwa mwaka 1993 kwa jukumu la Uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari ukanda wa SADC.
No comments:
Post a Comment