CWT WATOA KONGOLE KWA RAIS SAMIA KUJALI MASILAHI YA WALIMU
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
CHAMA wa Walimu Tanzania (CWT)
wameridhishwa na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia
Suluhu Hassan katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili walimu hapa
nchini ikiwemo masilahi na mazingira rafiki kazini.
Leah Ulaya,Rais wa chama wa
Walimu Tanzania(CWT) alitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Mei 2,2023 siku moja
baada ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani
Morogoro.
“Ninapenda kwa niaba ya
taasisi ninayoiongoza,na walimu wote,nitumie fursa hii kumpongeza na kumshukuru
Mama yetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa hotuba nzuri, yenye hamasa na kutia
moyo kwa walimu wote nchini”Alisema Leah Ulaya Rais wa CWT.
Alisema kuwa walimu
wameguswa sana na hutuba ya Rais Samia ambayo iligusa mambo muhimu na nyeti sana,kwa
mustakabali wa walimu na elimu nchini,kwamba katika hotuba hiyo iligusa utatuzi
wa wazi kwa baadhi ya changamotoambazo walimu walikuwa nazo.
Rais wa CWT taifa,Leah Ulaya,akihamasisha walimu wimbo wa mshikamano wakati alipoongea na waandishi wa habari Mjini Morgoro,Mei2,2023.
Katu Mkuu wa CWT taifa,Japhet
Maganga alisema walimu wamekuwa na matumaini makubwa kwa serikali ya Awamu ya Sita
chini ya Rais Samia kwamba imekuwa ikijali masilahi mapana ya walimu ambapo
changamoto nyingi zinazowakabili walimu kwa kipindi kirefu zimeanza kutafutiwa
ufumbuzi.
Maganga alisema kuwa walimu
wamekuwa na mwamko mkubwa wa kushiriki shughuli mbalimbali za kiserikali,ambapo
robo tatu ya watu walioshiriki kwenye siku ya wafanyakazi walimu walitia fora
kwa kujitokeza kwa wingi ikiwa ni kuonesha kumuunga mkono Rais Samia.
Aidha,alitaja mambo kadhaa
ambayo walimu wameboreshewa toka Rais Samia kuingia madarakani miaka miwili
iliyopita ambayo ni pamoja na upandaji w madaraja na kubadilishia miundoya
utumishi kwa wote waliostahili,kuendeslea kuboreshwa kwa miundombinu ya elimu
ikiwemo ujenzi wa madarasa.
Alitaja mengine ni pamoja
na kutoa ajira mpya 13,000,ugawaji wa vishikwambi kwa walimu wote,kwamba ahadi
iliyotolewa na Rais Samia katika hotuba yake kwa wafanyazi ya kuendelea
kupandisha madaraja kwa walimu,nyongeza ya mishahara ya kila mwaka,posho ya
kufundishia na utoaji wa ajira mpya kwa walimu zitatekelezeka kutokana na kasi
ya utendaji wake wa kazi toka aingie madarakani.
Jumanne Nyakirang’ani ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Morogoro kwa upande wake amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuonesha dhamira yake ya kuwaheshimisha walimu kusikiliza kero zao.
Rais wa CWT Taifa,Leah Ulaya akiongea na Waandishi wa Habari Mjini Morogoro
Nyakirang’ani alisema kuwa taifa lolote duniani haliwezi kupiga hatua
iwapo mchango wa walimu hautambuliwa na kuheshimiwa,hivyo kitendo cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuboresha masilahi ya
walimu ni jambo la kupongezwa sana.
Awali,Katibu wa CWT Mkoa wa
Morogoro,Alphance Mbassa alisema kuwa Walimu Mkoa wa Morogoro wanaupongeza
uongozi wa CWT taifa kwa kuonesha utashi wa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha kujali mchango wa
walimu hapa nchini.
Mbassa alisema kuwa hatua
ya uongozi wa CWT taifa kuweka program ya kutoa shukran kwa Rais Samia ni somo
kwa wadau wengine kuendeleza utamaduni huo ili kuleta umoja na mshikamano.
No comments:
Post a Comment