Denis
Msanzya Mjasiriamasli aomba, Huruma kwa Rais Samia
Na mwandishi wetu
UPO
msemo
wa wahenga usemayo “Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo”,ndivyo unavyoweza
kuelezea mkasa uliomkumba Mjasiriamali,Denis
Mathew Msanzya (55) mkazi wa Manispaa ya Morogoro aliyeingia mwenye
mkwamo wa kibiashara baada ya kushindwa
kubeba mzigo kodi wa zaidi ya milioni 202,huku akitegemeaa turufu moja ya
kupata huruma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu
Hassan kujinusuru kwenye kadhia hiyo.
Msanzya anamtaja Rais
Samia kuwa ni Kiongozi mashuhuri Barani Afrika na duniani kutokana kusimamia
haki,muumini wa maridhiano,mwenye falsafa ya kustawisha taifa,kiunganishi
cha makundi yote bila ya ubaguzi
wakiwemo wajasiriamali wenye viwango tofauti
za kibiashara.
Anasema katika uongozi
wake wa awamu ya sita, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ni Kinara kwa kuongeza
msukumo kwa wafanyabiashara wakubwa,wafanyabiashara wa ngazi ya kati na
wajasiriamali kuwa na moyo wa kizalendo kwa kutambua umuhimu wa kuchangia
mapato ya serikali bila ya kusukumwa kwa kulipa kodi.
Katika vipindi cha
miezi michache toka alipoingia madarakani kwa Rais Dkt.Samia, kuanzia mwezi
Julai hadi mwezi Desemba 2021 kiasi cha
shilingi trilioni 11.11 kilikusanywa Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Rais Samia kwa kukusanya
mapato kwa njia rafiki.
Mjasiriamali,Denis
Mathew Msanzya ni miongoni mwa wadau wa maendeleo anayemuunga mkono Rais Samia
kutokana na falsafa yake hiyo kwa maelekezo aliyoyatoa kwa Mamlaka ya mapato ya
kuwaelimisha umma kulipa kodi kwa hiari na kuondokana na dhana iliyojengeka
katika jamii ya ulipaji kodi ni adhabu.
“Mamlaka ya Mapato Tanzania
walipoutangazia umma kwamba ndani ya kipindi cha miezi mitatu kutoka julai hadi
Desemba 2021 walifanikiwa kukusanyaji kodi ya mapato zaidi ya trillion 11
iliningia akilini kwamba sasa TRA wamelielewa somo la Rais Samia kukusanya
mapato si kwa mabavu,njia rafiki ni mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi usio na
karaha.”Alisema Mjasiriamali Msanzya.
Akitoa uzoefu wake,
Msanzya anasema mfumo uliokuwa ukitumiwa siku za nyuma wa ukusanyaji kodi kwa
wafanyabiashara ulikuwa ni kero, lugha ya vitisho na baadhi ya maafisa wasio na
uadilifu walifikia hatua ya kuwataka baadhi wafanyabiashara watoe “kitu kidogo’
mfanyabiashara asipotekeleza walijikuta wakibambikiziwa madeni ya kodi.
MJASIRIAMALI,DENIS MATHEW MSANZYA AKIWA KATIKA MWONEKANO TOFAUTI
Anasema toka serikali ya awamu ya sita kushika msukani kero za wafanyabiashara zimeanza kushughulikiwa hii ni kutokana na kuwepo mazingira rafiki ya ulipaji wa kodi tofauti na siku za nyuma ambapo wafanyabiashara na wajasiriamali walilazimika kufunga biashara na hivyo kukosesha serikali mapato.Mjasiriamali Denis
Msanzya ni mzaliwa wa kijiji cha fam 28 (Kalemela) kilichopo,kata ya
Muungano,tarafa ya Urambo, Mkoa wa Tabora anasema katika safari yake ya kujitafutia kipato
ilianzaa baada ya kumaliza elimu yake ya msingi huko Tabora aliamua kushiriki
kwenye shughuli za kilimo cha zao la Tumbaku na mazao mengine.
Anasimulia safari yake
ya kujitafutia kipato, ilianza kuwa na viashiria ya mafanikio mara alipofika
mkoani Morogoro alipopata eneo la kuishi na sehemu ya kufanyia biashara ya duka
kama ilivyokuwa na ndoto yake aliyotoka nayo Tabora.
Anabainisha kwamba
alijiona ni mwenye bahati kwa kile alichokieleza alipata eneo la kufanyia biashara
zake baada ya kufuata taratibu zote za kisheria kuwa na leseni ya biashara, akapatiwa
namba ya mlipa kodi (TIN) ni 104870082 katika ofisi ya mamlaka ya mapato mkoa
wa Morogoro na kufungua duka la kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari,sembe,sigara
na majani ya chai.
Katika mazingira asiyoyatarajia mwaka 2009 alijikuta
akiingia kwenye sintofahamu alipokutwa
na maofisa wa TRA akishusha mzigo wa sukari mifuko 100 kwenye stoo ya duka
lake,mzigo huo ulikuwa na thamani ya shilingi mil.5400,000 aliyoinunua
kupitia wakala wa Kampuni ya Sukari ya
Kilombero Al Naeem.
Alisimulia kisa mkasa
hicho kilichomkututa siku ya tukio majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni
wanaume wawili walifika kwenye stoo ya bidhaa zake lililopo katika duka lake eneo
la Nunge wakati huo vijana walikuwa wakishusha sukari kwenye gari na kuingiza
stoo,watu hao awali hakuwatambua walikotoka na walikuwa wakihaji kitu
gani,walianza kuzozana na vijana waliokuwa wakishusha sukari wakiamuru waache
kufanya hivyo.
Kutokana na mzozo
huo,alilazimika kusimama kwa kuchechemea kwa msaada wa magongo kutokana na
ajali ya pikipiki iliyosababisha kuvunjika mguu wake wa kushoto,aliwaita watu
hao na kutaka kuwajua wao ni kina nani na wahitaji kitu gani,ndipo
walipojitambulisha kuwa wao ni maafisa wa TRA wametumwa na meneja wao wa Mkoa
kufika dukani hapo kwa ajili ya kufuatilia uhalali wa bidhaa hiyo iliyokuwa
ikishushwa.
Msanzya alielezea kutokana
na kauli hiyo alilazimika kutoa nyaraka za kupokea mizigo (Delivery order) na
kuwakabidhi maafisa wa kodi ambazo zilionesha
kuwa sukari hiyo imetolewa na kampuni ya sukari ya Kilombero kwenda kwa Al
Naeem.
Msanzya alidai alitoa
maelezo kwa maafisa hao kuwa bidhaa hiyo
ya sukari aliinunua kupitia kwa wakala wa bidhaa hiyo ambaye ni Al Naeem kwamba utarabu waliokuwa wakiutumia ni kufanya
malipo kwa njia ya benki kumbukumbu zote zimedhihirisha uhalali wa biashara
hiyo,baadae Maafisa hao walisogea pembeni walijadiliana kwa muda mfupi kisha wakarudi eneo lililokuwa nimeketi.
Alisema kuwa maafisa
hao wakampa taarifa kwamba nyaraka aliyokutwa nayo yaani ‘delivery order’
hazikuhalalisha uhalali wa bidhaa hiyo kwa kuwa alikosa risiti ya manunuzi.
Kutokana na sintofahamu
hiyo,aliletea notisi ya kutakiwa kulipa shilingi mil.6647244.40 pamoja na riba
baada ya kubainika kuwa na kosa la kuko la kununa bidhaa bila ya kuwa na
risiti,hivyo kuipotezea Serikali mapato na kukiuka sheria ya VAT 1997 Kifungu
na 40 na 47.
Aidha,toka wakati huo
aliendelea kuwasiliana na ofisi ya TRA Mkoa wa Morogoro kwa njia ya maandishi
ikiwemo barua bila ya kupata ufumbuzi huku
aliendelea kuuguza mguu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Ilipofika tarehe 10
Machi, 2011 anaeleza katika hali hiyo ya kibiashara,aliandika barua kwa meneja
wa TRA mkoa wa Morogoro kumtaarifu kuyumba kwa biashara yake na kusudio la
kufunga kwa biashara.baadae uongozi wa TRA mkoa wa Morogoro,ulituma maafisa
wake kufanya tathmini ya bidhaa zilizokuwa kwenye duka lake na kuwa na thamani
isiyozidi mil.64.5,akalazimika kufunga duka na kuanza na kwenda Tabora thamani
ya bidhaa zilizokuwepo dukani ni kiasi hicho jambo ambalo asingeweza kuhimili
kulipa deni hilo mil 188,207,476.00.
Katika mazingira hayo
ya kuyumba kibiashara alilazimika kurudi Tabora kuendelea na shughuli zake za
awali ya Kilimo fursa hiyo aliitumia kwa ajili ya kumtembelea Mama yake Mzazi
aliyekuwa mgonjwa.
Mwaka 2014 Msanzya
alirudi tena Morogoro kuendelea na biashara, aliunda kampuni ya Mjasiriamali
Investment Ltd.alisema ndoto yake ya kuwa mjasiriamali mkubwa imefifia na
kujikuta Kampuni yake ya Mjasiriamali
Investment Ltd ikiyumba na kuifunga licha ya kuwa amekuwa ikilipia kodi zake vizuri tangu
ilipoanzishwa mpaka mwaka 2015, TRA Morogoro walipotoa makadirio makubwa ya
shilingi 6,007,444.20 ambaye hayakuwa yanaendana na mapato ya Kampuni uongozi
wa Kampuni uliandika barua ya kupinga makadirio hayo na kuamua kufunga
biashara.
“Mchango wangu katika
ulipaji wa kodi kwa mwaka ni shilingi laki sita lakini baada ya miezi sita kodi
waliipatindisha hadi milioni sita kwa mwaka alilipa moja tu,hali hiyo imenilazimu
kampuni kuyumba na hatimaye kuifunga” alisema.
Sambamba na makadirio
ya kodi kwa Kampuni ya Mjasiriamali Investment Ltd, TRA Morogoro walimtolea
makadirio mengine ya kodi biashara iliyokuwa imefungwa na kutolewa taarifa kwa
maandishi TRA kuwa biashara imefungwa.Katika makadirio hayo Mjasiriamali huyo
alitakiwa kulipa Kodi kiasi cha shilingi 188,207,476.63.
Alifafanua kisha hicho
kilichotolea miaka 14 iliyopita akinukuu waraka uliotoka ofisi ya mapato mkoa
wa Morogoro kwamba kodi ya ongezeko la thamani alichotakiwa kukilipa kuanzia Januari-2009-2011
ni kiasi cha sh.161,201,708.33,
Kadhalika Kodi ya
mapato ya mwaka 2009 kiasi alichotakiwa kukilipa ni sh.3,838,343,30 huku kodi
ya mapato 2010/2011 kiasi alichotakiwa kukilipa ni shilingi 11,569,161.20,na
kufikia kiasi cha ya shilingi 188,207,476,63.
Aidha akiwa katika
dimbwi la kutafakari deni hilo, ilipofika tarehe 9/3/2017 akiwa kwenye gari
aina ya Noah yenye namba ya usajili T850 DDC iliyokuwa ikimilikiwa na mtoto
wake aliyemtaja kwa jina la Charles Denis Msanzya alijikuta gari hilo likikamatwa kwa kile alichoelezwa
na maafisa wa TRA ili kufidia deni hilo la shilingi188,207,476,63.
Msanzya akielezea mkasa
huo gari hilo lilishikiliwa na TRA kwa siku 33,baada ya kufuatilia kuwa gari
hilo halihusiani na analodaiwa na
hatimaye gari hilo likaachiwa.
Miezi saba baadae
ilipofika tarehe 20/11/2017 notisi ya madai walileta nyongeza (interesting ya
deni hilo) shilingi mil.14,603,358.na kusababisha deni hilo kuongezeka na kufika shilingi mil.202,833,300.71 hali yake ya kibiashara
ilizidi kumweka kwenye wakati mgumu kibiashara. (barua ya takukuru) na kuelekea
kufilika.
Aliwahi kuandika barua
ya kupinga makadirio ya kodi, kwa lakini alijibiwa kuwa pingamizi yake ya
makadirio ya kodi ilikuwa imechelewa,juhudi nyingine alizowahi kuzichukua
katika kukabiliana na changamoto hizo kuandika kwa Kamishna wa kodi za
ndani,aliwahi kufika kwa Naibu Katibu mkuu wa fedha ambaye alielekeza
malalamiko hayo yawasilishwe kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
lakini mpaka sasa toka mwaka 2019 hajapata majibu yoyote.
“kwa sasa nimekuwa nina
la kufanya,siwezi kufanyabiashara nimefilisika,pengine kupitia maelezo yangu,
ujumbe wangu utamfikia Rais Samia nikimuomba anisaidie suala hili lipatiwe
ufumbuzi.”Alisema Msanzya.
Alitaja athari
zilitozokea kutokana na hali hiyo ni kuyumba kimaisha,watoto kukosa haki yako
ya kusoma huku afya yangu ikitereka na kupata ugonjwa wa moyo na ambapo kwa
sasa anatimiwa hospitali ya Benjamini Mkapa,akihudhuria kliniki kila baada ya
mwezi.
Alisema anatamani
kufanyabiashara ili aendelee kuchangia ujenzi wa taifa,lakini kwa kuwa hana tax
clearance anashindwa kufanya chochote kwa kuwa asingeweza kulipa deni hilo
ilhali hafanyi biashara.
Alishauri Kamishna mkuu
wa mamlaka ya mapato Tanzania aweke utaratibu wa kutembelea kwenye mikoa
kusikiliza kero za wafanyabiashara ikiwa ni hatua ya kuwaweka karibu
wafanyabiashara waweze kulipa kodi bila ya shuruti kama maelekezo ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu anavyoagiza.
No comments:
Post a Comment