'WAFANYAKAZI’
SHIRIKA LA MZINGA WAMUOMBA RAIS SAMIA
Na.Mwandishi wetu
WALIOKUWA
wafanyakazi 15 wa Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro ambao waliofukuzwa
kazi kwa kosa la ujazaji wa fomu ya OPRAS kwenye kumbukumbu za elimu zao wamemuomba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan baada ya kukosa
ufumbuzi kwenye malalamiko yao kutoka mamlaka za chini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Dkt.Samia hivi karibun alitoa msamaha kwa wafanyakazi waliokuzwa
kazi kutokana na kuwa na vyeti feki kupewa mchango yao asilimia 5 waliychangia
kwenye mifuko ya kijamii lakini hali hiyo ni tofauti kwa kundi hilo la watu 15.
Ni Miaka 5 sasa toka kundi hilo
la wafanyakazi waliofukuzwa kazi na mwajiri wao lakini licha ya kuwepo nyaraka
mbalimbali zinazoeleza kurudisha kazini lakini hakujapatiwa ufumbuzi.
Erick Mshana, Carol Temba
na Yusuph Mbonde wakiongea kwa niaba ya wenzao,walidai kuwa msingi wa kumuomba Rais Samia awasaidie kutokana
na maelekezo yaliyowahi kutolewa na Katibu mkuu utumishi ofisi ya manejimenti ya
watumishi wa umma na utawala bora kwa waajiri wote nchini na wakuu wa taasisi
kupitia barua yenye kumb.na.CFB.228/290/01 “Y”/44 ya tarehe 24 septemba 2018 5 (B),
(C), (D) na (E) inayofafanua juu ya sakata la wafanyakazi kurejereshwa kazini
na kupewa stahiki zao.
“Mimi awali niliajiriwa nafasi ya dereva msaidizi nikiwa na elimu ya darasa la saba baadae nikapandishwa daraja na kuwa dereva nilihudumu kwa miaka 14 lakini nilifukuzwa kazi kwa madai ya kukosa kujaza fomu ya OPRAS kuwa anaufulu wa kidato cha nne”
“Tulijiendeleza elimu ya
sekondari kwa kufanya mtihani wa QT ingawa hatukufaulu lakini tukajikuta
tunafukuzwa kazi na mwajiri kwamba tumeghushi taarifa zetu jambo si kweli.”Yusuph Mbonde
Maelekezo ya serikali ni
kwamba ilitakiwa kuhakikiwa index namba ikiwa ni kuthibitisha kufanya mitihani
tajwa kwamba walitakiwa kurudishwa kazini kama watumishi wengine.
Waathirika wao walifukuzwa
kazi kati ya mwaka 2017 hadi 2019 wamemuomba Rais Samia kuingilia kati sakata
lao ambalo limegubikwa na sintofahamu baina ya waathirika hao na mamlaka za chini kushindwa kulipatia ufumbuzi.
Walidai kuwa watumishi wenzao
waliokuwa na sifa hizo katika shirika hilo walirudishwa kazini isipokuwa wao,
walilazimika kufuatilia bila ya mafanikio hadi sasa,kwamba wao waliajiriwa kwa
sifa za darasa la saba kabla ya Mei,2004 kwamba walijiendeleza kwa elimu ya sekondari
lakini hawakufaulu.
Erick Mshana ambaye
alifanyakazi kwa miaka 29, alisemai kuwa awali serikali ilitoa msamaha kwa wale
waliojiendeleza kielimu katika kiwango cha elimu ya baada ya kutokea
sintofahamu hiyo wamelazimika kupekea maombi yako kwa Rais Samia ili kuangalia
uwezekano wa kuomba suala hiyo ili liweze kupatiwa ufumbuzi kwa kadri ya
changamoto zao.
“kosa tunalotuhumiwa kwenye ujazaji wa fomu za
OPRAS inayotaka kueleza kiwango cha elimu,tulijaza kiwango cha elimu ya
sekondari baada ya kujiendeleza licha ya kuwa hatukufaulu kwamba hakuna nyaraka
yoyote ya kughushi kwenye taarifa zetu za ajira.”Alisema Mshana.
Aidha,Carol Temba alidai
kuwa zoezi hilo lilifanyika tofauti na ilivyotarajiwa kwani baadhi yao walirudishwa
lakini wao walifukuzwa kazi na waliendelea kufuatilia kwa miaka mitano sasa
bila ya mafanikio.
Walidai ya kuwa kilio chao ni cha muda mrefu lakini mpaka sasa licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali ili kutafuta haki zao bado juhudi hizo hajaleta mafanikio,hivyo wameomba Rais Samia awasaidie ili kupata haki zao kurudishwa kazini na stahiki zao kama walivyowa tumishi wengine nchini waliorudiwa kazini.
No comments:
Post a Comment