FUNDI WA JENGO LA CHOO ZAHANATI YA MALIPULA,CHAMWINO,hamwino adai fidia mil.8,250,000
Na Mwandishi wetu,Morogoro
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Morogoro huenda ikafikishwa mahakamani iwapo fidia ya shilingi mil 8,250,000
hakitalipwa kufuatiwa kukiukwa kwa mkataba wa ujenzi wa wagonjwa katika zahanati ya Malipula iliopo
Kata ya Chamwino mjini humo.
Kusudio hilo la kuifikisha
Manispaa ya Morogoro Mahakamani limetokana na Adrian Mugalula ambaye ni fundi
wa ujenzi aliingia mkataba wa ujenzi wa jengo la choo na miundombinu ya maji
taka na maji safi na mganga mfawidhi wa zahanati ya Malipula kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ambapo
mkataba mnamo mei 26,2021.
Mugalula alidai ya kuwa kwa
upande wake alitimiza wajibu wake kama fundi katika kipindi chote cha mkataba
lakini ilipofika hatua za mwisho ya kukamilisha ujenzi hupitia utaratibu wa ‘force
account’ bila ya kupata maelezo kutoka upande wa ofisi ya Mganga Mfawidhi wa
zahanati hiyo wakasitisha utoaji wa fedha za ujenzi kinyume na mkataba.
“baada ya kuona hali hiyo
niliwasilisha na mwanasheria wangu na kupeleka hoja zangu ofisi ya Mkurugenzi
wa Manispaa ili kushughulikia suala langu kinyume cha hapo ninakusudia
kuishitaki manispaa ya Morogoro.”Alidai Mugalula.
Hata hivyo,pamoja na
kupeleka kusudio hilo mpaka sasa hakuna
kinachoendelea hali ambayo inazua sintofahamu kwa Mugalula na hivyo kulazimika
kuanza mchakato wa kufikisha madai yake kwenye vyombo vya sheria.
Akitoa mchanganuo wa madai
yake Mugalula anaidai manispaa shilingi 75,000 gharama za kuwalipa mafundi
wasaidizi,fundi mkuu shilingi 3,875,000,usafiri wa mafundi kutoka sangasanga
hadi eneo la kazi(chamwino) sh.93,000,gharama za maji 38,000 na kufanya gharama
halisi ya uvunjwaji wa mkataba ni sh.4,005,000 huku gharama nyingine za
usumbufu ikitadaiwa ni shilingi 4,245,000 na kufanya jumla kuu ya fedha
zinazodaiwa kulipwa na manispaa ya Morogoro ni shilingi mil.8,250,000.
Hata hivyo,uchunguzi uliofanywa
umebaini ya kuwa mpaka sasa hakuna shauri lolote lililofunguliwa dhidi ya
manispaa ya Morogoro kuhusiana na madai hayo.
Wadau wa maendeleo kutoka
kata ya Chamwino ambao hawakupenda majina yao yachapishwe alisema kuwa suala
hilo linaweza kuzungumzika iwapo pande zote mbili zikakaa meza ya mazungumzo
kwa masilahi mapana ya pande zote kupitia upya vipengele vilivyopo kwenye
mkataba badala ya kukimbilia mahakamani.
No comments:
Post a Comment