WAANDISHI
WA HABARI MORO WAJENGEWA UWEZO ELIMU,MAFUTA NA GESI ASILIA
Na Loveness Nyawili,Morogoro
JUMLA ya
waandishi wa habari 16 kutoka vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Morogoro wamepatiwa
semina utendaji wa kazi wa shirika la maendeleo ya Petroli na Tanzania(TPDC)
ikiwa ni mkakati maalum wa ushirikishwaji wa wadau unaoendeshwa na shirika
hilo.
Semina hiyo imefunguliwa na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga alisema kuwa waandishi wa habari
wanajukumu kubwa la kupasha habari kwa umma hivyo Shirika la TPDC kimefanya
uamuzi sahihi wa kuwapa elimu waandishi wa habari.
Kihanga alisema kuwa juhudi
zinazaofanywa na serikali za kuwaletea maendeleo wananchi haziwezi kufahamika
vema iwapo vyombo vya habari havitatimiza wajibu wao,hivyo alitoa wito kwa
waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema katika kuhabarisha umma.
Alisema kuwa matumizi ya
gesi asilia kama nishati mbadala itapunguza ukataji wa miti na kuchochea
matumizi ya nishati safina kuwezesha wananchi kuwa na afya bora na kuepukana na
uchaguzi wa mazingira na kuifanya kuifanya nchi kuwa jangwa.
BAADHI WAANDISHI WA HABARI WALIOSHIRIKI KATIKA SEMINA HIYO WAKIWA MAKINI KUFUATILIA SEMINA HIYO WA KWANZA KULIA NI NICKSON MKILANYA,MWENYEKITI MOROPC,JACOB SONYO KATIKATI MWANDISHI WA HABARI AYO TV NA SIFUNI MSHANA MWANDISHI ITV (PICHA NA LOVENESS NYAWILI)
Katika hotuba yake Mstahiki
meya alisema kuwa taarifa zilizopo sasa zinaeleza kuwa Mikoa ya Morogoro na
Pwani vimekuwa vinara wa ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa hivyo ni jukumu la
waandishi wa habari kuwasaidia wananchi kuacha ukatajiwa miti na badala yake
wananchi wapande miti ili kuepuka jangwa.
Katika semina hiyo
waandishi wa habari wakiongozwa na mwenyekiti wao Nickson Mkilanya wa chama
chao cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro(Morogoro Press Club) walipitishwa kwenye mada mbalimbali fursa
zilizopo katika mkondo wa juu na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya
TPDC,gesi asilia na fursa zake katika mkondo wa kati na chini ya petrol na
mradi wa bomba la mafuta ghafi la afrika mashariki(EACOP).
Asiad Mrutu ni meneja mradi
wa TPDC alisema kuwa serikali ya Tanzania imetoa kiasi cha shilingi bilioni 267
ikiwa ni mchango wake katika utekelezaji
wa mradi wa EACOP kupitia shirika la maendeleo ya petrol Tanzania.
Mrutu alisema alibainisha
baadhi ya maendeo ya mradi hupo yaliopo nchini Tanzania lot 2 yenye kilombera
614 kutoka Mtukura hadi singida na kuhusisha vituo vya pampu 4,vituo vya umeme
8 na kambi za ujenzi 7 huku lot 3 ikuhusisha kilombeta 533 kutoka Mkoa wa
Singida Tanga ambapo kutakuwa na vituo 2 vya kupunguza msukumo(PRS),vituo vya
umeme 6 na kambi za ujenzi 7.
Kwa upande wake,Eva Swillah
Afisa TPDC alitaja viwanda vya kuchakata gesi asilia ni
PAET-songosongo,M&P-Mnazi bay,TPDC-Madimba,TPDC-Songosongo ambapo asilimia
70 ya umeme unaozalishwa na Tanesco unatokana na gesi asilia.
Sallah pia alibainisha kuwa
gesi asilia inatumika katika kuendeshea mitambo viwandani ambapo viwanda
vipatavyo 53 na nyumba takribani 1500 vimeunganishwa katika mtandao wa gesi
asilia kwa matumizi ya kupikia majumbani huku ikikadiriwa kuwa magari 1500
yanatumia gesi asilia katika kama nishati mbadala wa petrol na dizeli.
No comments:
Post a Comment