UTPC SASA KUELEKEA
JIJINI DODOMA, YAHAMISHA OFISI YAKE JIJINI MWANZA
Na Mwandishi Maalum,Dar
VIONGOZI wa Klabu za waandishi wa Habari
nchini Tanzania,wamekutana jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano maalum huku
kukiwa na ajenda ya kuwepo mabadiliko ya katiba ya umoja wa Klabu za waaandishi
wa habari (UTPC) ikiwa ni mkakati wa utekelezaji wa kauli mbiu ‘good
to great.’
Kwa mujibu wa waraka wa mkurugenzi mtendaji wa Klabu za
waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) Kenneth Simbaya kwa viongozi wa Klabu
alisema mkutano huo ni licha ya kuwa ni mkutano wa kawaida lakini umelenga
kuweka mikakati ya kuleta mabadiliko chanja kwa kufuata kauli mbiu ya kuipeleka
taasisi ya UTPC kutoka hali nzuri kuelekea hali nzuri zaidi.
Mbali ya hayo,wajumbe wa mkutano mkuu uliofanyika Desemba
6,2022 katika ukumbi wa millennium tower 2- Kasenga,wamefikia azimio la
kuhamisha makao makuu ya UTPC kutoka Jijini Mwanza na kuhamia makao makuu ya serikali
Jijini Dodoma.
Wakati huo huo,Simbaya alibainisha ya kuwa mbali na agenda hizo pia kutakuwa na hafla maalum ya kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa UTPC,Abubakar Karsan ambaye alihudumu kwa uadilifu taasisi hiyo kwa miongo kadhaa na kuleta mafanikio makubwa ya Klabu za Waandishi wa habari ambayo chini ya rais wake Deogratius Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoma Press Club.
No comments:
Post a Comment