Na Lilian Lucas, Morogoro
MKUU wa
mkoa wa Morogoro Fatuma Mwasa amesema mbolea ni moja ya pembejeo muhimu katika
kuongeza tija ya uzalishaji hivyo matumizi ya mbolea bora yanahitajika ili
kuongeza mavuno na malighafi mbalimbali zinazotumika viwandani.
Amesema hayo mjini Morogoro
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya udhubiti ubora wa mbolea kwa wadhibiti kutoka
mikoa 19 ya Tanzania bara yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
Tanzania(TFRA).
Alisema katika kuelekea
uchumi wa viwanda, mahiyaji ya malighafi ambayo kwa zaidi ya asilimia 70 ni
mazao ya kilimo yataongezeka sana na kwa vile maeneo ya uzalishaji yatabaki
vilevile ni wazi kwamba kuna kila njia ya kuongeza tija ya uzalishaji.
Aidha, Mwasa amesema katika
miaka mitano iliyopita Tanzania imekuwa ikitumia mbole kati ya tani 300,000 na
500,000 za mbolea aina mbalimbali kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 30-50 ya
lengo la kutumia tani 1 milioni kwa mwaka.
Mkuu huyo wa moa wa
Morogoro amesema mkakati wa kuongeza matumizi ya mbolea kwa sasa umekuwa na umuhimu wa kipekee
hasa ikizingatiwa kwamba serikali imeweka
lengo la kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya uchumi unaotegemea viwanda.
Amewataka wadhibiti hao
ubora baada ya kuhitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia mwongozo maalumu wa
udhibiti ubora wa mbolea(Standard Operating Procedure(SOP) for Fertilizer
Quility Assurance Officers in Tanzania) ambao umeandaliwa mahususi kwa ajili
yao.
WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UDHIBITI WA MBOLEA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Aidha, amesema pamoja na
uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo wafanyabashara wachache ambao hufanya
vitendo mbalimbali vya kupunguza ubora wa mbolea kwa kujua ama kutojua jambo
linalopelekea mbolea kupungua ubora wake ni vyema hatua za kisheria
zikachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara hao.
Kaimu mkurugenzi mtendaji
wa TFRA Happness Mbelle amesema tfra imeendelea kushirikiana wadau mbalimbali
katika mnyororo wa thamani wa mbolea ili kuhakikisha mbolea inayopatikana
nchini inatosha na inakuwa na ubora uliokusudiwa , huku ikiimalisha mawasilino
kati ya Serikali na wadau wengine wa mbolea.
Mbelle amesema mamlaka
imekuwa ikifanya kaguzi kushirikiana na maafisa wa halmashauri kwa ajili ya
kuhakikisha mbolea zilizopo sokoni zinaendelea kuwa na ubora unaotakiwa, pamoja
na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya mbolea nchini ili upatikanaji unakuwa
wa kutosha.
Vilevile, amesema mwaka
2022/2023 Serikali imetoa sh 150 milioni kwa ajili ya ruzuku ya wakulima na
TFRA ni chombo kilichokasimiwa madaraka kwa ajili ya kuhakikisha ruzuku
inakwenda sawa na lengo kuu ni kupunguza makali ya bei ya mbolea kwa wakulima
na kuongeza uzalishaji wa tija katika kilimo, kuhakikisha usalama wa chakula
nchini na kuongeza malighafi kwenye viwanda.
Pia, amesema lengo kuu ni
kutengeneza wadhibiti ambao watakuwa wanafanya kaguzi katika maduka na sehemu
mbalimba ili kuhakikisha mbolea inayopatikana inakuwa ya ubora wa kutosha.
Mbelle amesema mpaka sasa
wadhibiti 140 wamepatiwa mafuzno na wanaendelea kufanya kazi na halmashauri.
No comments:
Post a Comment