Na Mwandishi wetu,Dodoma
MAKAMU wa
Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi
wa Habari Tanzania (UTPC) Bi Pendo Mwakyembe ametoa wito kwa viongozi wa Klabu
za wanahabari nchini kuongoza kwa kuzingatia misingi ,Kanuni na katiba zao.
Wito huo umetolewa Jijini
Dodoma hivi Karibuni katika mafunzo ya uongozi na Usimamizi wa fedha kwa
viongozi wa klabu yaliyowakutanisha wenyeviti ,Makatibu,waweka hazina ,waratibu
na wajumbe wa kamati za utendaji kutoka mikoa mitano ili kuboresha klabu zao
kuwa na uongozi bora.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa kamati ya fedha na Mipango wa (UTPC) ambaye pia ni Katibu mtendaji wa Chama
cha Waandishi wa Habari Morogoro (MOROPC) Bi.Lilian Lucas Kasenene amehimiza
viongozi wa klabu kutatua changamoto zinazojitokeza katika vyama vyao ikiwemo
migogoro ndani ya vyama huku akibainisha kuwa ripoti mbalimbali za ukaguzi na
tathmini ambazo UTPC imefanyiwa na taasisi za Delloite na FCG zinaonyesha
mapungufu na namna ya kukabiliana nazo ili kuleta uimara ndani ya taasisi.
Naye, Afisa programu na
Mafunzo wa UTPC Bwana Victor Maleko ameeleza kuwa ni vyema klabu za waandishi
kutumia fursa za mafunzo hayo kwa kufungua ukurasa mwingine wa kutumia uzoefu
uliopatikana kwenda kubadili mifumo ili kuondosha migongano katika uongozi
ulipo
Mafunzo hayo
yamewakutanisha viongozi kutoka mikoa ya Morogoro ,Katavi,Mbeya,Songwe na Rukwa
No comments:
Post a Comment