Breaking News

Dec 31, 2022

RC MWASSA ATAKA WAANDISHI KUJIKITA HABARI ZA UCHUNGUZI

 MKUU WA MKOA WA MOROGORO FATMA MWASSA AKITOA HOTUBA KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MOROGORO(MOROPC)

RC MWASSA ATAKA WAANDISHI  KUJIKITA HABARI ZA UCHUNGUZI

Na Mwandishi wetu

MKUU wa Mkoa wa Morogoro,Fatma Mwassa ametoa wito kwa waandishi wa habari mkoani hapa kuandika Habari za uchunguzi zitakazosaidia kuzipatia ufumbuzi changamoto ya migogoro ya ardhi sambamba na mapigano baina ya wakulima na wafugaji.

Mkuu wa Mkoa Fatma alitoa rai hiyo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Morogoro,uliofanyika Desemba 30,mwaka huu,na kungoza kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuhakikisha wanaandika kwa kina habari zitakazoleta suluhu ya kwenye migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara mkoani hapa.

Alisema kuwa njia pekee ya kutafutia suluhu ya changamoto hiyo ni kuwa na mkakati wa pamoja utakahusisha wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari ambao kutokana na taaluma waliokuwa nayo itasaidia kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuepuka matumizi ya ardhi kiholela na kuzingatia sheria badala ya kurubunika na madalali wanaotoa hati feki.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka idara mbalimbali za serikali wakifuatilia kwa karibu Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Fatma Mwassa(hayupo pichani)

Aidha,alisema mbali na changamoto za migogoro ya ardhi,watu kuvamia kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo msitu wa kuni uliopo eneo la Kiegea mpakani mwa wilayani mvomero na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Alisema pia Mkoa wa Morogoro una changamoto ya kuwepo kwa matukio ya ukatili wa kijinsia huku akinyooshea kidole jeshi la polisi morogoro kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia na utoaji wa taarifa za matukio hayo kwa wakati ili watuhumiwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Baadhi ya wanachama wa Morogoro Press Club wakifuatilia kwa karibu hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano mkuu wa wanachama wote

Nickson Mkilanya ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro ametoa ahadi kwa mkuu wa mkoa kwamba kwa niaba ya waandishi wa habari mkoani hapa watamuunga mkono ajenga ya serikali katika kupambana na migogoro ya ardhi,matumizi holela ya rasiliamali ardhi yanayosababisha uwepo wa migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro,Nickson Mkilanya akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa katika Mkutano mkuu wa Wanachama wa MOROPC

Mkilanya alisema kuwa Klabu ya waandishi wa habari Morogoro ina uzoefu katika kushughulikiwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa njia shirikishi kutoka na kuwahi kutekeleza mradi wa elimu shirikishi kwa umma katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kutokana na umuhimu wa ajenda  hiyo na mpango mkakati maalum unaondaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro itarajia kutoa tuzo kwa waandishi wa habari watakaojikita katika kufanya utafiti juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi,migogoro ya wakulima na wafugaji na jinsi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Katibu Mtendaji wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro Lilian Lucas ambaye pia ni Mjumbe wa bodi ya UTPC akitoa maelezo juu ya umuhimu wa Mkutano huo kwa wanachama.

 Wajumbe wa Mkutano wa huo walipitisha kwa kauli moja maazimio ya mkutano mkuu wa UTPC uliofanyika Desemba 17 jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuifanya Taasisi mwavuli wa Klabu za waandishi wa habari kutoka hali njema kuelekea hali njema zaidi.

No comments:

Post a Comment