CCM
MOROGORO MJINI KUWAPA USHIRIKIANO WAANDISHI WA HABARI
Na Loveness Nyawili
KATIBU wa Chama cha
Mapinduzi,Morogoro Mjini,Amiri Mkalipa amesema CCM ina tambua mchango wa
waandishi wa habari katika kuhamasisha
utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa wananchi kupitia miradi ya kimkakati inayoendelea katika maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Mkalipa alibainisha hayo
wakati alifanya mazungumzo na uongozi wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa
Morogoro(MOROPC) Desemba 27,2022 alipofanya ziara yake ya kutembelea Taasisi na
wadau wa maendeleo ikiwemo Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro.
“Waandishi wa Habari kama
muhimiri wa nne wana nafasi kubwa ya kuhabarisha,kukosoa ikiwa ni kuonesha njia
sehemu ambayo yenye changamoto ili wenye mamlaka waweze kuzipatia ufumbuzi.”Alisema
Alisema ofisi yake ipo
tayari kushirikiana na waandishi wa habari kama wadau wakuu wa maendeleo
kutokana na mchango mkubwa wanaoutoa katika kuhamasisha maendeleo na kufichua
uovu katika ngazi ya jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro,Nickson Mkilanya alionesha
kufurahishwa na hatua iliyofanywa na kiongozi huyo wa chama kwa kile
alichokieleza kwamba ni viongozi wachache wenye mtazamo chanya kwa waandishi wa
habari.
Mkilanya alisema kuwa wapo
baadhi ya viongozi wamekuwa na mtazamo hasi kwa kuwaona waandishi wa habari ni
maadui na hata wakati mwingine wamekuwa wazito kutoa ushirikiano kwa waaandishi
wa habari hasa suala la utoaji wa taarifa zenye masilahi mapana kwa umma.
Aidha,Mkilanya
amemhakikishia Kiongozi huyo kuwa waandishi wa habari watatoa ushirikiano wa
kutosha kwa ofisi yake na kuwa mahusiano kati ya waandishi wa habari na
wanasiasa ikiwemo ofisi ya chama hicho ngazi ya wilaya ya Morogoro mjini.
Alielezea pia mkakati wa
maendeleo ya chama cha waandishi wa habari kwamba ni kuendeleza uwekezaji
unaendana na mazingira yaliopo ikiwa ni sehemu ya kuleta chachu ya maendeleo
kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro.
Lilian Lucas ni Katibu
Mtendaji wa MOROPC alisema pamoja na jitihada za kuhakikisha ya kuwa mahusiano
kati ya waandishi wa habari na wadau yanaimarika lakini zipo changamoto kwa
baadhi ya taasisi za kiserikali zimekuwa hazitoi ushirikiano wa kutosha katika
utoaji wa taarifa kwa wakati.
Lilian alisema kuwa hatua ya kiongozi huo kufanya ziara katika ofisi za waandishi wa habari zimefungua ukurasa mpya ambao utakuwa ni mfano wa kuigwa kwa wadau wengine ili kuwahudumia wananchi bila ya kuwepo kwa vikwazo visivyo vya lazima.
No comments:
Post a Comment