SHIRIKA
LA SWISSCONTACT YATOA FURSA KWA WAKAZI WA MOROGORO
Na Mwandishi wetu
WADAU wa
Maendeleo,Shirika la Maendeleo la kimataifa,Swisscontact wanatarajia kutoa
fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi ikiwa ni
mkakati wa kuwajengea uwezo vijana kujiajiri.
Shirika la Swisscontact lililopo
mjini Morogoro wamekuwa wakitumia njia shirikishi katika utekelezaji wa program
zake mbalimbali wakilenga kushirikiana na serikali na wadau wengine kukabiliwa
na changamoto kubwa za maendeleo katika masuala ya kuchumi na ukosefu wa ajira
na elimu kwa vijana.
Nickson Mkilanya ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro(MOROPC) ametoa maelezo mara baada ya kukutana na wadau hao wa maendeleo Januari 11,mwaka huu na kufafanua ya kuwa wanufaika na mradi inayotekelezwa na Shirika la Swisscontact ni vijana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 24.
NICKSON MKILANYA KUSHOTO AKIONGEA NA MAAFISA WA SHIRIKA LA SWISSCONTACT“Twaweza kuiita ni neema
kwa mkoa wa Morogoro baada ya Shirika la Maendeleo la kimataifa la Swisscontact
kuupa mkoa wa Morogoro nafasi ya kuwa kati ya mikoa michache itakayonufaika na
uwepo wake nchini Tanzania katika utekelezaji wa mradi ya aina hiyo.”Alisema Mkilanya.
Mkilanya alisema kuwa mradi utakayowanufaisha vijana ni pamoja na uwezeshaji na uafutaji wa soko la ajira
kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 24,sanjari na kuwajengea uwezo zaidi wa ufundishaji kwa
walimu wa vyuo vya maendeleo (FDC).
Baadhi ya vyuo vya maendeleo (FDC) vilivyopo Mkoa wa Morogoro ni pamoja na Bigwa,Kilosa na Ifakara huku mikoa mingine itakayonufaika na miradi hiyo ni Mkoa wa Iringa na Mbeya ambapo mradi wa aina hiyo utazinduliwa hivi karibuni pia utatekelezwa katika vipindi vya miaka minne minne.
No comments:
Post a Comment