WALIMU 600 MVOMERO WADAI
MALIMBUKIZO YA MISHAHARA
Na. Thadei Hafigwa,Morogoro
JUMLA ya
Walimu mia sita wilaya ya Mvomero,mkoa
wa Morogoro wanadai serikali malimbikizo ya mishahara tangu mwaka 2014 bila ya
mafanikio hali inayopunguza ari ya utendaji wao wa kazi.
Katibu wa Wilaya ya
Mvomero,Herry Kavalambi alibainisha hayo katika mkutano mkuu wa wanachama na wawakilishi viongozi mahala pa kazi
uliofanyika katika ukumbi wa Umwema JKT, jana na kuongeza kuwa walimu wamekuwa
wakiondolewa kwenye mishahara bila kuzingatia taratibu za kazi na utumishi wa
walimu.
Kavalambi alisema kuwa
mbali na changamoto walizokuwa nazo
walimu pia kutolipwa madeni ya fedha za likizo pamoja na upungufu wa
miundombinu mbalimbali shuleni ikiwemo samani,nyumba za walmu,vyoo vya walimu
nawanafunzi.
Aidha,alisema kuwa chama cha walimu wilaya ya mvomero hawakupaliani na mfumo mpya wa kikotoo kwa kuwa ni gandamizi na sio rafiki kwa wafanyakazi hivyo ameiomba serikali kuandalia upya kikokotoo hicho kwa masilahi mapana kwa umma.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa viongozi wawakilishi mahala pa kazi chama cha walimu Tanzania(CWT),Wilaya ya Mvomero“kikotoo kilichoanza
kutumika mwezi julai 2022 si rafiki kwa wafanyakazi sisi hatukubaliani nacho ni
kikotoo gandamizi ndio maana baadhi ya wafanyakazi wamejistaafisha haraka
kukwepa kikotoo hicho gandamizi”Alisema Kavalambi ambaye pia ni kaimu katibu wa
chama cha walimu mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo,Kavalambi
ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jitihada za kuwapandisha madaraja
walimu na ujenzi wa miundombinu ya madarasa na kuwafanya wanafunzi kuwa katika
mazingira bora ya kujifunzia.
Kwa upande wake,Mwenyekiti
wa chama cha walimu Wilaya ya Mvomero Jonas Maliashamba alisema kuwa chama
hicho wilayani kwake inakabiliwa na ukosefu wa jengo lake kwamba walimu
wanalazimika kusafiri umbali mrefu mkoani kupata huduma na kuathiri ratiba na shughuli
nyingine za kitaaluma katika maeneo ya kazi.
Maliashamba alisema ili
kukabiliana na jambo hilo wanahitaji kuungwa mkono na uongozi wa cwt makao
makuu kwa kuwa tayari wanamiliki kiwanja chenye ukubwa wa ekari 4 katika
kufanikishwa kuwa na jengo lake.
Mkutano huo uliofunguliwa na Jane Mtindya,Mjumbe wa tume ya utumishi wa Umma kupitia shule za sekondari nchini, aliahidi kuzifikisha changamoto hizo katika vikao vya ngazi ya kitaifa ili ziweze jadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Akijibu risala ya walimu Mtindya alisema kuwa suala ya kikotoo ni suala mtambuka hivyo changamoto nyingine za kisera zitajadiliwa katika ngazi ya kitaifa kwa kuendelea kufanya mazungumzo na serikali ili kuangalia namna bora ya kuwaondolea walimu changamoto zinazowakabili.
Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Mvomero,Herry Kavalambi (kulia) akiteta jambo na mwekahazina wake,Golden Katoaliwakumbusha walimu kuzingatia maadili na kanuni za ajira kutokana na kuwepo matukio yanayofanywa na baadhi ya walimu wasio waadilifu kukiuka kanuni za utumishi wa umma na kuzorotesha ufanisi katika kazi.
Alisema kuwa takwimu walizonazo zinaonesha kuwa zaidi ya walimu 1000 wameshapoteza kazi kutokana na makosa mbalimbali lakini asilimia 75 katika makosa hayo ni utoro kazini,kwamba walimu wamekuwa wakiondoka katika sehemu zao za kazi bila ya kutoa taarifa kwa mwajili wao.
Alihimiza walimu kushikamana na kukumbushana bila kushoka misingi mitatu inayosimamia taaluma ya ualimu kwamba utoaji wa taaluma kwa wanafunzi,makuzi ya kimwili na kiroho jambo ambalo ndiyo kiini cha kupewa heshima kwamba ualimu ni wito tofauti na taaluma nyingine.
No comments:
Post a Comment