VIONGOZI WALIMU WANAWAKE ‘WAPIGANA MSASA’ SHERIA ZA KAZI
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
CHAMA
cha walimu nchini kimeendesha mafunzo kwa walimu viongozi wanawake ikiwa ni moja
ya mkakati wa kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika masuala ya sheria za kazi
na sheria mbalimbali za nchi sanjari na kujitokeza kugombea nafasi za uongozi
wenye vyombo vya maamuzi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika
Mjini Morogoro, Oktoba 8 na 9,2022 na kufunguliwa Kaimu Rais wa Chama Cha Walimu
(CWT),Dinah Mathaman ambapo imewakutanisha walimu wanawake viongozi kutoka
mikoa yote iliyopo Tanzania bara,
Elizabeth Werema ni wakilishi
wa walimu wanawake taifa,alisoma risala kwa niaba ya wenzake alisema kuwa
kitengo chao pamoja na mafanikio waliopata lakini wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti za kuendesha shughuli zao pamoja na ukosefu
wa akaunti yao katika ngazi ya kitaifa.
Elizabeth alisema kuwa
kitengo chao kimeonesha imani kubwa kwa viongozi kutoka na juhudi wanazofanya
zilizosababisha kuongeza matumaini kwa wanachama na kuongeza marejesho ya Mikoa
na Wilaya.
Aidha,alipongeza viongozi
kamati tendaji taifa na baraza la taifa kwa kutenga bajeti japo hatoshi
kulingana na mpango Mkakati walio nao kushindwa kutekelezwa kwa wakati, hivyo
aliomba kwa mwaka mwingine bajeti ya kitengo hicho iongezwe ili kurahisha
utendaji kazi wao.
Hata hivyo,kitengo
kinatambua juhudi za viongozi katika kubainisha malengo na madhumuni ya uwepo
wa kitengo kama ilivyoabinishwa na viongozi wa chama kwenye katiba,kanuni na
sera ya jinsia na walimu wanawake.
Alisema mwaka 2013
walianzisha sera ya jinsia na walimu wanawake wajumbe wa kamati mbalimbali katika
matayarisho ya uanzishwaji wa sera ya jinsia na walimu wanawake iliweka dira
kwamba ifikapo mwaka 2025 CWT iwe na wanachama wenye maarifa,ujuzi,ujasiri
katika kutetea usawa wa jinsia ili walimu wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika
vyombo vya maamuzi na uongozi katika
ngazi zote.
Alisema mafunzo hayo yawashirikisha walimu wanawake viongozi nchini kote ambapo jumla ya washiriki 135 ili kupata maarifa na kufanya tathmini ya mfanikio na changamoto walizonazo hususan kitengo cha walimu wanawake.
Hata hivyo alisema kuwa hali
ya kitengo walimu wanawake kipo imara kwamba wanaendelea na shughuli zao kwa
kuzingatia vikao vya kikatiba,vikao vya dharura,huduma kwa wanachama, ziara kwa wanachama, semina na warsha na mafunzo
sanjari na kushiriki kwenye maadhimisho mbalimbali katika ngazi ya kimkoa na
kitaifa.
“huduma kwa wanachama
zinafanywa kwa kiasi kikubwa zinafanywa na kitengo cha walimu wanawake kwa
kushirikiana na viongozi wa ngazi zote wilayani,kimkoa na kitaifa”Alisema
Alitaja baadhi huduma
wanazozitoa ni pamoja kuwahudumia walimu wagonjwa na waliopata kadhia
mbalimbali ikiwemo kushiriki katika kutatua migogoro kati ya wanachama na
wanachama au wanachama na mwajiri yanayohusiana na masuala ya kijinsia.
Kuhusu Changamoto Elizabeth katika risala yao zinazowakabili
kitengo cha walimu wanawake pamoja na kukosekana kwa kasma inayojitegemea ndani
ya chama cha walimu na kusababisha kupata bajeti ndogo hali inayowalazimu
kunyanganyana na bajeti inayotengwa katika ngazi ya wilaya na mkoa hivyo
kudhorotesha utendaji kazi kwa ufanisi.
Huku akipiga chepuo kurudishwa
kwa asilimia 20 ya gharama za utendaji wa shughuli za kitengo chake kwenye
ngazi ya wilaya na Mkoa,bila kuathiri utendaji wa kitengo maalum,kadhalika
aliomba CWT makao makuu kufanya maamuzi ya kimkakati ya kuwafungulia akaunti ya
kitengo chao kama ilivyo kwenye Wilaya na Mkoa.
Akijibu risala hiyo,Kaimu
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania,Dinah Mathaman alisema ofisi yake
itawasilisha hoja hizo katika kamati tendaji ili changamoto hizo ziweze
kupatiwa ufumbuzi.
Mathaman aliwakumbusha
walimu wanawake kujitambua, kujiamini na kuwa na moyo wa uthubutu kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya uamuzi.
alisema kazi iliyofanywa na
walimu wanawake katika kuhakikisha walimu wanajisajiri kwenye chama ni kazi
inayotakiwa kupongezwa kwamba ofisi yake itahakikisha ya kuwa kitengo hicho
kinawezeshwa ili kuleta matokeo makubwa kwa siku zijazo.
Alisema kuwa wamekuwa na
maadili mema kwa kuonesha jamii kuwa na mwelekeo bora na kukubalika katika
jamii ili kuhakikisha taifa linasonga mbele.
Alisema wanawake wamekuwa wakishiriki kwenye nafasi mbaimbali za uongozi ikiwa ni moja ya kutua ya kuleta chachu ndani ya CWT na nje ya chama cha walimu.wapate ujasiri na kujiamini na kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Kaimu Rais wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Dinah Mathaman(hayupo pichani).Alisema mwanamke akisimama
katika nafasi mbalimbali imekuwa na matokeo chanja kutokana na tafiti
mbalimbali zilizofanywa na wanazuoni ndani na nje ya nchi.
Aliahidi kuhakikisha ya
kuwa asimilia 20 iliyokuwa ikitengwa kwa ajili ya kitengo cha walimu wanawake
kinarejeshwa na kurahisisha katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake,Kaimu
Katibu mkuu CWT Taifa,Japhet Maganga aliwasihi walimu wanawake kuwa mstari wa
mbele bila ya kuchoka katika kusimamia malezi katika ngazi ya familia ili
kunusuru hali ya mmomonyoko wa maadili uliopo hapa nchini.
Aliwakumbusha kusimamia
sera ya wanawake na badala ya kutegemea viongozi na kuepuka kwenda kwa matukio
ili uimarisha kitengo cha wanawake walimu hivyo kujitokeza kwenye kugombea
nafasi ya uongozi.
Alisema ni vema kuwahimiza
wajibu wao kwa mwajiri,familia,na malezi inapaswa kila mmoja kujitathmini namna
ya kulitimiza lengo la kulea familia na taifa kwa ujumla.
Alisema ni vema
kushirikiana na viongozi wanawake wanamiliki mali na kushimamia mirathi
kikamilifu.kutumia elimu katika kutimiza wajibu na utatuzi wa migogoro katika
maeneo wanayotoka kutokana na ujasiri na uvumilivu waliokuwa nao.
Aliwasa walimu kujiendeleza
kitaaluma na hivi sasa walimu wamekuwa na ari ya kujifunza na kujiendeleza
kielimu kwamba jukumu hilo ni kuwahimiza wengine walikuwa wazito katika
kuongeza elimu.
Aliwaasa walimu
kuwaelimisha wengine hasa walimu wanawake waweze kushiriki kwenye masuala ya
ujasiriamali ili kuongeza kipato cha ziara ili kutatua changamoto ndogondogo zilizopo
katika ngazi ya familia.
Aliwasa walimu kujitathmini
katika kuendesha nyimbo za hamasa kwenye vyombo vya habari ikiwemo luninga na
redio.
Naye,Mwenyekiti wa chama
cha walimu Mkoa wa Morogoro,Jumanne Nyakirang’ani alisema kuwa jukumu waliopewa
viongozi wa chama cha walimu ni kuwahudumia wanachama kwa kutumia rasilimali
zilizopo kwa ushirikiano wa pamoja.
Alisema kuwa Wanawake ni
nguzo ya mambo yote,kwamba bila mama hakutakuwa na hatua za kwenda,mwanamke
popote alipo ni mama,mwanamke ni rafiki,huku akinukuu sehemu ya mtunzi wa shairi
la Fitina kwamba “Fitina titi la paka halifai kuwa mtindi,fitina ngozi
ya tembo halifai kwa kuwambwa”
Alisema kuwa CWT ilifikiwa
hatua ya kwenda hali jojo kutokana na kuwepo kwa viashiria vya fitina hivyo
aliwaasa wale wote wenye ‘tabia ya
uchawa’ kuachana na mwenendo huo na badala yake kuilinda taasisi hiyo kwa kuwa ni
inategemewa na wengi na imetoa ajira kwa wengi kote nchini.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliotolewa
kwa walimu viongozi kitengo cha walimu wanawake wa chama cha walimu,kimelenga
zaidi kuwaongezea uelewa juu ya sheria za
kazi pamoja na sheria za nchi, kutambua tume za utumishi wa walimu na kazi
zao,kupata maarifa ya kuandishi wa taarifa na kuongeza ujuzi katika masuala ya
uongozi.
No comments:
Post a Comment