Baadhi ya washiriki wa
mkutano mkuu wa chama cha walimu Kilosa wakiongozwa na viongozi wa chama
hicho,ngazi ya Wilaya,Mkoa na Wawakilishi wa Taifa.
WALIMU KILOSA WAHAMASIKA
KUJIUNGA NA BENKI YAO
Na Thadei Hafigwa
MWENYEKITI wa
chama cha walimu Wilaya ya Kilosa Richard Shagungu amesema kuwa
walimu wilayani humo wamehamasika katika kujiunga na benki ya walimu licha ya
kuwepo kwa changamoto zinazoikabili benki hiyo.
“Ninatoa wito kwamba watendaji wa benki hiyo kuendelea kutoa
hamasa kwa kutembelea wilayani ili walimu waendelee kuwa na imani kwa benki
yao”Alisema
Aidha,Shagungu alisema wilaya yake ina mipango mbalimbali ya
kimaendeleo ili kuwapunguzia changamoto za walimu ikiwemo usafiri ikiwa ni
mkakati wa kuhakikisha ya kuwa walimu wanakuwa katika mazingira mazuri katika
utendaji wa kazi zao.
Shagungu katika mpango mkakati huo alibainisha ununuzi wa gari kwa
ajili ya kuwasaidia walimu wilayani huo wanapopata msiba na matatizo mengine ya
kijamii waweze kuzikabili kwa haraka.
wajumbe wa mkutano huo,walipitisha mpango wa ununuzi wa gari kwa
kauli moja huku wakijiwekea lengo la mwaka mmoja kukamilisha mpango huo ili
uwanufaishe walimu wilayani Kilosa na hivyo kuwa chachu ya maendeleo ya walimu
katika mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Kilosa,Richard Shagungu
alisema ofisi yake kabla ya kuwasilisha hoja ya ununuzi wa gari walifanya
utafiti na kubaini ya kuwa walimu wanapopata msiba licha ya kupewa stahiki na
mwajiri wao lakini wamebaini kuna huduma za haraka zingeweza kutatuliwa iwapo
wangekuwa na gari.
Shagungu alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 61 zitatumika
katika kugharamia ununuzi wa gari la walimu Wilaya ya Kilosa,ambapo itakuwa ni
Wilaya ya kwanza kwa mkoa wa Morogoro kumiliki gari.
Katika mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali katika ngazi ya wilaya,Mkoa na wawakilishi wa taifa,ambapo kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Morogoro,Jumanne Nyakirang’ani alitumia mkutano huo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kuwapandisha madaraja ya walimu na kulipa madeni yaliyokuwa wakidai kwa kipindi kirefu.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa
wa Morogoro,Jumanne Nyakiran'gani kushoto akitoa hotuba yake katika mkutano
mkuu wa Chama cha walimu Wilaya ya Kilosa
Nyakirang’ani alisema kuwa licha ya mazingira magumu lakini
wamekuwa wakifanyakazi kwa uweledi na kusaidiana na serikali katika kampeni
mbalimbali ikiwemo sense ambapo walimu walifanyakazi kwa uweledi mkubwa.
Alisema kuwa,walimu wamekuwa nadhifu wakati wakitoka nyumbani lakini wanapofika mazingira ya shuleni wachafuka hivyo iwapo azima ya serikali itaendelea ya kuweka mazingira mazuri ya kujenga nyumba za walimu itasaidia kuboresha mazingira bora kwa walimu nyumbani na shuleni.
Aliwaasa walimu wakati wa kusimamia mitihani ya darasa la saba kwa
uadilifu ili kupata wanafunzi waadilifu kwa kufanya mitihani yao bila ya
udanganyifu.
Katika Mkutano huo pia wajumbe walifanya uchaguzi mwakilishi wa
vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC) ambapo kwa Wilaya yaKilosa
aliyejitokeza kugombea nafasi hiyo alikuwa ni mmoja Mwalimu Ginslar Ngonyani
Lulinda kutoka chuo cha maendeleo ya wananchi Kilosa.
Kaimu Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Morogoro (CWT) Herry Kavalambi,ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza Mwalimu Ginslar Ngonyani Lulinda kuwa mwalikishi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi kwa kuchaguliwa kura 192 ,kura 4 ziliharibika na kura za hapana zilikuwa 13 kati ya kura 219 za wajumbe wote wa mkutano mkuu huo.
No comments:
Post a Comment