MARUFUKU
MWANDISHI WA HABARI KUVUNJIWA VITENDEA KAZI-DC MSANDO
MKUU wa Wilaya ya Morogoro
Albert Msando, amezitaka Taasisi za serikali na halmashauri kuwapa ushirikiano
waandishi wa habari kupata taarifa kwa wakati bila ya kuwepo na urasimu.
Msando alitoa rai hiyo Septemba 11,2022 wakati akifungua mdahalo kati ya wajumbe wa ulinzi na usalama na waandishi wa habari uliofanyika katika Bwalo la Umwema JKT ambapo aliwahakikisha waandishi wa habari kwamba kamati ya ulinzi na usalama wilaya ipo tayari kushirikiana na waandishi wa habari na kwamba amekemea vikali tabia ya kuwanyanyasa waandishi wa habari katika wilaya yake ambapo pia aliwapongeza waandishi wa habari kufanya kazi kwa uweledi.
“Ni marufuku kwa taasisi na
watumishi wa halmashauri kumzuia waandishi wa habari kutimiza wajibu wao,pia
wasivunje kamera,simu au vitendea kazi,na badala kutumia njia ya
kueleweshana”Alisema.
Alisema kuwa waandishi wa
habari wanafanyakazi kubwa sana katika kuripoti taarifa za maendeleo ili
kuharakisha maendeleo ya wananchi waishio pembezoni.pia aliwakumbusha waandishi
wa habari kuhakikisha ya kuwa wanatekeleza majukumu yao bila hofu kwa kuwa
serikali ya awamu ya sita imeongeza uhuru wa kujieleza.
Alisema kuwa waandishi wa
habari wasiandike habari zitakazoleta taharuki lakini pia wasiache kukosoa
pindi inapojitokeza kuna ukiukwaji wa
maadili ya utumishi,kwamba kalamu yao inasaidia serikali kutambua kuwa kuna
mambo yanafanyika na watumishi walio na uadilifu.
Aidha,Mkuu wa Wilaya aliwataka waandishi wa habari kuendelea kuripoti habari za maendeleo ya wananchi kupitia miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa bwawa la fufua umeme Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo sehemu ya mradi huo upo kwenye wilaya yake.
“Kusoeni kwa staha na
hakuna mtu atakayewazuia kufanya hivyo,lililo la msingi ni kuzingatia sheria na
katiba ya nchi ili kila mtu aweze kupata haki zake za msingi za kupata taarifa na
kutoa maoni yenye kuleta tija”Alisema Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambaye pia ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
Awali Mwenyekiti wa Klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Morogoro,Nickson Mkulanya alimshukuru Mkuu wa
Wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuonesha utayari wao wakati wote
wa kufanyakazi na waandishi wa habari Morogoro.
Mkilanya alimhakikishia
mkuu wa Wilaya kwamba waandishi wa habari wa
morogoro wapo tayari kufanyakazi usiku na mchana katika kuhamasisha
maendeleo ya wananchi hususan waliopo
pembezoni.
katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na katibu tawala wa Wilaya ya Morogoro Bi Ruth John ambaye aliwakumbusha waandishi wa habari kutochoka kufanyakazi licha ya mazingira magumu waliokuwa nayo.
Bi.Ruth aliwapongea waandishi wa habari wa Morogoro ambao baadhi yao wamekuwa wapo mstari wa mbele katika wamekuwa wakijitoa kuwahudumia wananchi bila ya kujali ni mazingira gani yaliopo,mjini na vijijini,wenye kipato na wasio na kipato.
No comments:
Post a Comment